IKULU ya Afrika Kusini imetangaza kuwa Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na mpigania haki nchini Afrika Kusini, Askofu Desmond Tutu amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.
Taarifa ya ofisi ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa imeeleza kuwa Rais amesikitishwa na kifo hicho na kwa niaba ya raia wote wa Afrika Kusini anatoa pole kwa mke wa Askofu Tutu na familia nzima ya askofu huyo.
Rais Cyril Ramaphosa amesema kwamba kifo cha muhudumu huyo wa kanisa kimeadhimisha kwa mara nyengine misiba ya kizazi muhimu cha taifa hilo .
Alisema kwamba Askofu Tutu alisaidia katika kurithi taifa la Afrika kusini lililokombolewa .
Tutu alikuwa mmojawapo ya viongozi maarufu nchini humo na Ugenini.
Alishiriki katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi akishirikiana na Nelson Mandela, na kuchochea harakati za kukomesha sera ya ubaguzi wa rangi iliyotekelezwa na serikali ya wazungu wachache dhidi ya weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kuanzia 1948 hadi 1991.
Alitunukiwa tuzo ya Nobel mwaka 1984 kwa jukumu lake katika mapambano ya kukomesha mfumo wa ubaguzi wa rangi.
Kifo cha Tutu kinajiri wiki chache tu baada ya Rais wa mwisho wa enzi za ubaguzi wa rangi FW de Clerk , kufariki akiwa na umri wa miaka 85.
Rais Ramaphosa alisema kwamba Tutu alikuwa kiongozi maarufu wa dini , mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi na mpiganiaji wa haki za binadamu kote duniani.
Alimuelezea kuwa mtu mzalendo , kiongozi mwenye misimamo aliyetoa maana kwa ufahamu wa Biblia kwamba imani bila matendo ni sawa na kifo.
"Alikuwa mtu mwenye ufahamu wa ajabu, mwadilifu na asiyeweza kushindwa dhidi ya nguvu za ubaguzi wa rangi, pia alikuwa mpole na mwenye huruma kwa wale ambao walikuwa wamepitia dhuluma na vurugu chini ya ubaguzi wa rangi, mbali na watu waliokandamizwa kote ulimwenguni."
Alitawazwa kama padre mwaka wa 1960, na kuhudumu kama askofu wa Lesotho kuanzia 1976-78, askofu msaidizi wa Johannesburg na mkuu wa parokia ya Soweto.
Alikua Askofu wa Johannesburg mnamo 1985, na akateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza mweusi wa Cape Town. Alitumia nafasi yake ya hadhi ya juu kuzungumzia ukandamizaji dhidi ya watu weusi nchini mwake, siku zote akisema nia yake ni ya kidini na si ya kisiasa.
Desmond Tutu alikuwa askofu aliyekuwa na tabasamu na misimamo iliowavutia marafiki na wengi waliomuenzi duniani.
Akiwa kiongozi wa mweusi wa dini mwenye umaarufu mkubwa duniani , alihusika sana katika harakati dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache lakini akasisitiza kuwa lengo lake kuu lilikuwa la kidini na sio kisiasa.
Aliteuliwa na rais Nelson Mandela kuongoza tume ya ukweli na maridhiano ilioundwa kuchunguza uhalifu uliotekelezwa na pande zote mbiIi wakati wa enzi za ubaguzi wa rangi
Pia alisifika kwa kuanzisha neno taifa la Rainbow kuelezea mchanganyiko wa watu wa makabilay, rangi na dini tofauti nchi Afrika kusini . Desmond Mpilo Tutu alizaliwa 1931 katika mji mdogo wenye migodi ya dhahabu wa Transvaal.
Alifuata nyayo za babake kwa kuwa mwalimu , kabla ya kuwacha kazi hiyo baada ya kupitishwa kwa sheria ya elimu ya Bantu Education Act 1953 ambayo ilipinga ubaguzi wa rangi shuleni.
Alijiunga na kanisa na akapata ushawishi mkubwa kutoka kwa viongozi weupe wa dini nchini humo , hususan Askofu Trevor Huddleston aliyepinga sana unaguzi wa rangi.
Tutu (kulia) akiwa na wanachama wenzake wa chuo cha Pretoria Bantu Normal College mwaka 1961
Alihudumu kama askofu wa Lesotho kuanzia 1976-78, askofu msaidizi wa Johannesburg na mkuu wa parokia ya Soweto, kabla ya kuteuliwa kuwa askofu wa Johannesburg.
Alikuwa smkuu wa chuo ndipao alipoanza kupaza sauti yake dhidi ya ukosefu wa haki nchini Afrika Kusini na tena kuanzia 1977 alipokuwa katibu mkuu wa Baraza la Makanisa la Afrika Kusini.
Akiwa mtu mashuhuri kabla ya uasi wa 1976 katika vitongoji vya watu weusi, ilikuwa miezi kadhaa kabla ya matukio ya ghasia za Soweto ambapo alijulikana kwa mara ya kwanza na Wazungu wa Afrika Kusini kama mwanaharakati wa mageuzi.
Juhudi zake zilimfanya kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 1984 katika kile kilichoonekana kuwa pingamizi kuu dhidi ya jumuiya ya kimataifa kwa watawala weupe wa Afrika Kusini.
Kutawazwa kwa Desmond Tutu kama Askofu Mkuu wa Cape Town kulihudhuriwa na Askofu Mkuu wa wakati huo wa Canterbury, Dk Robert Runcie, na mjane wa Martin Luther King.
Akiwa mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Afrika Kusini, aliendelea kufanya kampeni kikamilifu dhidi ya ubaguzi wa rangi. Mnamo Machi 1988, alitangaza: "Tunakataa kuchukuliwa kama kifutioa miguu cha mlango ili serikali kufuta buti zake."
Miezi sita baadaye, alinusurika kifungo jela baada ya kutoa wito wa kususia uchaguzi wa manispaa.
Alikamatwa katika wingu la gesi ya vitoa machozi mnamo Agosti 1989, wakati polisi walichukua hatua dhidi ya watu waliokuwa wakitoka kanisani katika kitongoji kimoja karibu na Cape Town, na mwezi uliofuata alikamatwa baada ya kukataa kuondoka kwenye mkutano uliopigwa marufuku.
Desmond Tutu akiwa akitembelea mji chini ua uangalizi wa maafisa wa polisi
Akiwa askofu mkuu, wito wake wa vikwazo vya adhabu dhidi ya Afrika Kusini uligonga vichwa vya habari ulimwenguni kwasababu uliambatana na kulaani vikali ghasia
Mnamo 1985, Tutu na askofu mwingine kwa ujasiri na kwa kasi walimuokoa muhudumu wa polisi alipokuwa akishambuliwa na kukaribia kuchomwa hadi kufa na umati uliojaa ghadhabu katika kitongoji kimoja mashariki mwa mji wa Afrika Kusini, Johannesburg.
Makasisi hao waliusukuma umati huo na kumvuta ili kumlinda mwanamume huyo aliyekuwa akivuja damu, nusu-fahamu, kabla tu ya tairi iliyomwagiwa petroli shingoni kuwashwa.
Tutu baadaye aliwakemea washambuliaji wa mtu huyo, akiwakumbusha "umuhimu wa kutumia njia za haki kwa ajili ya mapambano ya haki ".
Tutu aliunga mkono mabadiliko yaliyotangazwa na Rais FW de Klerk mara baada ya kuchukua madaraka. Mabadiliko hayo ni pamoja na kuondolewa kwa marufuku kwa chama cha ANC na kuachiliwa kwa Nelson Mandela Februari 1990.
Muda mfupi baadaye, Tutu alitangaza kupiga marufuku makasisi kujiunga na vyama vya kisiasa, jambo ambalo lililaaniwa na makanisa mengine.
Kuhusu Israel na Palestina
Hakuwahi kusita kutoa maoni yake. Mnamo mwezi Aprili 1989, alipokwenda mjini Birmingham nchini Uingereza, alikosoa kile alichokiita "taifa mbili" Uingereza, na kusema kuna watu weusi wengi katika magereza ya nchi hiyo.
Baadaye aliwakasirisha Waisraeli wakati wa hija ya Krismasi kwenye ardhi hiyo takatifu, akiwalinganisha Waafrika Kusini weusi na Waarabu katika ukingo wa Magharibi na Gaza unaokaliwa kwa mabavu.
Alisema hawezi kuelewa ni vipi watu walioteseka kama Wayahudi wangeweza kuwasababishia Wapalestina mateso hayo.
Alijikuta katikati ya vitoa machozi wakati wa mkutano wa kupinga ubaguzi wa rangi
Desmond Tutu alimpenda sana Nelson Mandela, lakini hakukubaliana naye kila mara katika masuala kama vile matumizi ya vurugu katika kutafuta suluhu ya haki.
Mnamo Novemba 1995, Mandela, aliyekuwa rais wa Afrika Kusini wakati huo, alimwomba Tutu kuongoza Tume ya Ukweli na Maridhiano, yenye jukumu la kukusanya ushahidi wa uhalifu wa enzi za ubaguzi wa rangi na kupendekeza kama watu wanaokiri kuhusika kwao wanapaswa kupata msamaha.
Mwishoni mwa uchunguzi wa tume hiyo, Tutu aliwashambulia viongozi wa zamani wa Wazungu wa Afrika Kusini, akisema wengi wao walidanganya katika ushahidi wao. Tume hiyo pia ilishutumu ANC kwa kufanya ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa vita vyake dhidi ya ubaguzi wa rangi. Pande zote mbili zilikataa ripoti hiyo
Alibubujikwa na machozi
Tutu mara nyingi alishindwa na uchungu wa wale walioteseka chini ya ubaguzi wa rangi na, kwa zaidi ya tukio moja, alitokwa na machozi.
Alibubujikwa na machozi wakati wa ibada ya mwisho ya TRC 2003
He also found much to criticise in South Africa's new black-majority government. He launched a stinging attack on the ANC administration led by President Thabo Mbeki.
He said the ANC had not done enough to alleviate poverty among the poorest in the country and that too much wealth and power was concentrated in the hands of a new black political elite.
He later urged Jacob Zuma, who had been accused of sexual crimes and corruption, to abandon his attempts to become president.
Pia alikuwa na sauti kubwa katika kumshutumu Robert Mugabe, wakati mmoja akimuelezea rais wa Zimbabwe kama "mchoro wa katuni wa dikteta wa zamani wa Kiafrika". Mugabe, kwa upande wake, alimtaja Tutu kama "mwovu".
Mara nynegine angaweza pia kuwa mkosoaji wa kanisa lake la kianglikana hasa baada ya mzozo wa kuwekwa wakfu kwa maaskofu mashoga.
Milele mwasi
"Mungu analia," alisema wakati mmoja aliposhutumu kanisa kwa kuruhusu "mapenzi ya jinsia moja kuchukua nafasi ya kwanza juu ya vita dhidi ya umaskini duniani.
Alirejea katika suala la umaskini alipozuru Ireland mwaka 2010. Aliyataka mataifa ya Magharibi kuzingatia athari za kupunguzwa kwa misaada ya ng'ambo kutokana na kuzorota kwa uchumi.
Tutu alikuwa na jukumu kubwa katika sera ya Mandela ya maridhiano
Tutu alistaafu rasmi kutoka kwa maisha ya umma mwaka huo huo na, alisema, kutumia muda mwingi "kunywa chai nyekundu ya msituni na kutazama kriketi" kuliko "kukaa katika viwanja vya ndege na hotel
Lakini wakati wowote akiwa mwasi, alijitokeza kuunga mkono usaidizi wa kujiua mwaka 2014, akisema kwamba maisha hayapaswi kuhifadhiwa "kwa gharama yoyote".
Kinyume na maoni ya watu wengi wa kanisa, alishikilia kwamba wanadamu walikuwa na haki ya kuchagua kufa.
Alisema rafiki yake mkubwa na mwanaharakati mwenzake Mandela, ambaye alifariki Desemba 2013, aliugua ugonjwa wa muda mrefu na wenye uchungu ambao kwa maoni yake "ulikuwa dharau kwa utu wa Madiba".
Mnamo mwaka wa 2017, Tutu alimkosoa vikali kiongozi wa Myanmar na mshindi mwenzake wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi, akisema "ni jambo lisilofaa kwa ishara ya uadilifu" kuongoza nchi ambayo Waislamu walio wachache walikuwa wakikabiliwa na "maangamizi ya kikabila".
Alipokutana na mwanamfalme na binti mfalme wa Duchess of Sussex na mwana wao Archie wakati wa ziara ya yao Afrika Kusini 2019
Baadaye mwaka huo huo, alipinga uamuzi wa Donald Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu rasmi wa Israel. "Mungu analia," aliandika kwenye Twitter, juu ya kitendo hiki cha "uchochezi na kibaguzi".
Mwanamume mdogo, "Arch", kama alivyojulikana, alikuwa mkarimu na mpole, akitoka roho ya furaha licha ya hisia zake nyingi za utume.
Alikuwa mwerevu, na mazungumzo yake mara nyingi yalipuuzwa na kukejeliwa.
Lakini zaidi ya haya, Desmond Tutu alikuwa mtu mwenye imani thabiti ya kimaadili ambaye alijitahidi kuleta pamoja Afrika Kusini yenye amani.
CHANZO- BBC SWAHILI
Social Plugin