JESHI la Polisi nchini Kenya wanamshikilia Dereva Bodaboda kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Thaara ambaye walikutana nae Facebook.
Polisi wanasema wawili hao walikutana Facebook na kuanzisha urafiki na Mwanafunzi akasafiri kutoka Kijiji cha Kamahuha na akamfuata Mwanaume nyumbani kwake eneo la Gaturi ambako umauti umemkutia.
“Mwili utafanyiwa uchunguzi kujua kilichopelekea kifo cha mwanafunzi huyo, na tayari tunaendelea kuwahoji Majirani ambao wamekiri kumuona Mwanafunzi akiingia ndani kwa Bodaboda huyo,” imesema Polisi.
Social Plugin