Mbunifu wa mavazi na mitindo Bertha Komba (Kasikana)
Na Joel Maduka - Geita
Mbunifu wa mavazi na mitindo hapa nchini Bertha Komba (KASIKANA ) amesema ipo haja ya kufanyika utafiti wa kina na kuandika historia ya sanaa ya ubunifu wa mavazi kwa hapa nchi, ili kuifahamisha jamii sanaa ya ubunifu ilikuwaje hapo nyuma, hivi sasa na mueleko wake wa baadae.
Wito huo ameutoa wakati akizungumza na Malunde 1 blog ofisini kwake Mkoani Geita,baada ya kuibuka Mshindi wa Tuzo ya Ubunifu bora wa mavazi Afrika Mashariki kwenye tuzo ambazo zilikuwa zikitolewa Nchini Kenya Wiki iliyomalizika kwenye Jukwaa la Mitindo la Pwani International Fashion week and “
“Ni vizuri tukajua kwa miaka iliyopita jamii ya watanzania walikuwa wakivaa mavazi ya aina gani? na kwa staili ipi?walikuwa wakifungaje vilemba, ni vazi la aina gani lilikuwa likipendwa zaidi, na mambo kama hayo ili kujua kama khanga, kitenge au vazi gani lilikuwa bora kwa wakati ule” ,amesema Kasikana Mbunifu wa mavazi.
Kasikana ameongeza kuwa ni vyema sasa Nchi ya Tanzania ikatambua mchango wa wabunifu katika kuitangaza nchi na kikaundwa chombo mahususi ambacho kitakuwa na sera ambazo zinatawasimamia wabunifu katika shughuli zao kama ambavyo mataifa mengine yameendelea kufanya.
Sambamba na hayo, aliishauri serikali kupitia wizara ya utamaduni na michezo, kuandaa sera ya sanaa ya ubunifu wa mavazi itakayosaidia kutoa muongozo katika sekta hiyo na ya sanaa ya ubunifu ambayo inakuwa siku hadi siku hapa nchini.
Aidha mbunifu huyo wa mavazi aliongeza kuwa wasanii wa fani ya ubunifu wa mavazi wapatiwe fursa za kushiriki katika matukio mbailimbali yanayoandaliwa na serikali na taasisi mbalimbali kwani wanaowezo wa kutoa mchango mkubwa kufanikisha matukio hayo kupitia kazi zao.
Kasikana amekuwa ndani ya Tasnia ya ubunifu tangu 2014 na alianza kushiriki majukwaa ya mitindo nchini Kenya tangu 2017 hatimaye mwaka huu amejitwalia Tuzo ya Mbunifu Bora wa mwaka Afrika Mashariki.
Social Plugin