OFISA mmoja wa Jeshi la Polisi Naivasha nchini Kenya amemuua kwa kumpiga risasi bosi wake aliyemuuliza mbona alifika kazini kwa kuchelewa tena akiwa amelewa.
Joseph Muthunga alimmiminia risasi Ayub Polo katika kambi ya AAPS, Kedongo usiku wa Jumamosi kabla ya kutoroka na kukimbilia kusikojulikana.
Mabaki matano ya risasi yamekutwa eneo la tukio hilo lilitokea katika kambi ya AAPS eneo la Kedong, Naivasha
Makachero mjini Naivasha wameanzisha msako mkali dhidi ya mtuhumiwa huyo.
Inaelezwa kuwa Muthunga alifika kambini hapo akiwa amelewa na kuzua ugomvi na afisa mwenzake Sajenti Ayub Polo baada ya kuulizwa mbona alirejea kambini kwa kuchelewa ilhali alistahili kuwa kazini usiku huo.
Ugomvi huo ulitokea kuwa mkali sana ndipo Muthunga alipochukua bunduki aina ya G3 na kummiminia risasi Sajenti Polo kisha kukimbia mafichoni.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha ya risasi kwa sikio, bega na goti. Mabaki ya risasi tano yalipatikana katika eneo la tukio.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, Umme mjini Mai Mahiu unakosubiri kufanyiwa uchunguzi.
Social Plugin