Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA KIVULINI LASHINDA TUZO YA RUZUKU KINARA WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa pili kulia) akiwa amesimama wakati Shirika lake la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Kutetea haki za wanawake na Watoto - Kivulini lenye Makao yake Makuu Jijini Mwanza limeshinda Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia hususani katika Kutokomeza Mimba za utotoni na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Shirika la KIVULINI limepokea Tuzo hiyo leo Jumatano Desemba 8,2021 kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania katika Siku 16 za Uanaharakati Kupinga Ukatili wa Kijinsia‘A Joint Champions Award and Concert on 16 Days of Activism Against Gender Based Violence – with over 30 artists, sports champs and activists’ lililofanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam.

Mashirika sita yaliyotangazwa kuwa Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia likiwemo Shirika la KIVULINI yatapokea mchango wa Fedha zilizokusanywa katika tamasha hilo na mchango huo utaenda kusaidia jitihada zao za kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Tuzo hizo za Ruzuku ambazo zimeing’arisha KIVULINI Kimataifa zimeandaliwa na Taasisi za Umoja wa Mataifa ambazo ni UN Women, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) pamoja na Umoja wa Ulaya na Balozi mbalimbali nchini Tanzania ambazo zimetambua juhudi zinazofanywa na Shirika la KIVULINI katika kutokomeza Mimba za utotoni na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Akizungumza mara baada ya KIVULINI kutangazwa kuwa Shirika Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema Tuzo hiyo ni ya haki kutokana na kazi kubwa wanayoifanya katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo wamefarijika kuona wapo watu wanatambua mchango wao na kuitangazia dunia.

“Tunaushukuru Umoja wa Ulaya na Taasisi za Umoja wa Ulaya na Balozi mbalimbali kwa kutambua mchango mkubwa wa shirika la KIVULINI pamoja na mashirika mengine matano kutoa Tuzo ya Kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia. Hii kwetu sisi itatupa ari zaidi, nguvu kubwa kwa kwenda sasa nyumba kwa nyumba, uvungu kwa uvungu na tutawekeza nguvu zaidi kwa wananchi na taasisi za kiserikali ili kuhakikisha athari za ukatili wa kijinsia hazinyamaziwi na kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko”,amesema Ally.

“Tuzo hizi zimetutia moyo na kutupa thamani kubwa kwa sababu kazi tunayoifanya inatambulika kitaifa na kimataifa. Tuzo inatupa nguvu mpya za kupambana na aina zote za ukatili zikiwemo mimba za utotoni, ndoa za utotoni kwa kuimarisha mapambano haya ambapo sasa tuna wanaharakati wa kujitolea zaidi ya 2000 na tunafanya kazi katika mikoa zaidi ya 6 yenye kiwango kikubwa cha ukatili”,ameongeza Ally.

Shirika la KIVULINI (Kivulini Women’s Right Organization - Mwanza) limetangazwa kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia , mashirika mengine ni Hope for Girls and Women in Tanzania (Mara), Agape Organization (Shinyanga), Tanzania’s Media Women’s Association (TAMWA) – Zanzibar, DMI Spring of Hope (Dar es Salaam) na Shika Ndoto (Dar es Salaam).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiushukuru Umoja wa Ulaya na Taasisi za Umoja wa Ulaya na Balozi mbalimbali kwa kutambua mchango mkubwa wa shirika la KIVULINI katika kupinga ukatili wa kijinsia na kulipa shirika lake Tuzo ya Ruzuku ambayo itakwenda kusaidia jitihada zao za kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akielezea namna tuzo ya Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia ilivyowapa thamani kubwa KIVULINI kwani kazi wanayoifanya inatambulika kitaifa na kimataifa. Amesema tuzo hiyo imewapa nguvu mpya za kupambana na aina zote za ukatili zikiwemo mimba za utotoni na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akielezea namna tuzo ya Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia ilivyowapa nguvu ya kwenda kuwekeza nguvu zaidi kwa wananchi na taasisi za kiserikali ili kuhakikisha athari za ukatili wa kijinsia hazinyamaziwi na kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa pili kulia) akiwa amesimama wakati Shirika lake la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania katika Siku 16 za Uanaharakati Kupinga Ukatili wa Kijinsia lililofanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa pili kulia) akiwa amesimama wakati Shirika lake la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa tano kushoto) akifuatilia matukio wakati Shirika la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (katikati) akifuatilia matukio wakati Shirika la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania
Wanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia wakiwa kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania ambapo shirika la KIVULINI limetangazwa kushinda tuzo ya Ruzuku kutokana na ukinara wake katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Msanii Ben Pol akitoa burudani kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania ambapo shirika la KIVULINI limetangazwa kushinda tuzo ya Ruzuku kutokana na ukinara wake katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Msanii Nandy akitoa burudani kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania ambapo shirika la KIVULINI limetangazwa kushinda tuzo ya Ruzuku kutokana na ukinara wake katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Wasanii mbalimbali wakitoa burudani kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania ambapo shirika la KIVULINI limetangazwa kushinda tuzo ya Ruzuku kutokana na ukinara wake katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com