Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASKOFU KINYAIYA AWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUISHI IMANI YA KRISTO NA KUENENDA KATIKA USAWA

 ASKOFU  Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Dodoma Mhashamu Beatus Michael Kinyaiya,akiongoza Misa takatifu ya Krismasi katika Parokia ya Mtakatifu Petro Mtume-Swaswa, sanjari na utoaji wa sakramenti ya Kipaimara kwa Vijana 60  wa Parokia hiyo.
*****

Na,Dotto Kwilasa-Malunde 1 blog, DODOMA.

ASKOFU  Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Mhashamu Beatus Michael Kinyaiya, amewataka  Watanzania  kuendelea kuwaombea Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan ili waweze kuongoza katika haki,usawa,umoja na .shikamano kama anavyofundisha Yesu Kristu mfalme wa amani.


Hayo amesema wakati akitoa Homilia yake kwenye Adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu Sherehe ya Kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristu,katika Parokia ya Mtakatifu Petro Mtume-Swaswa, sanjari na utoaji wa sakramenti ya Kipaimara kwa Vijana 60  wa Parokia hiyo.


Amesema maombi ya kuwaombea Viongozi wa nchi yanahitajika kwa kila mwananchi, ili Viongozi hao waliopewa mamlaka ya kuwaongoza Watanzania waweze kuyaishi maagizo yake.


"Kwa kipekee kabisa nawaomba wananchi wote, kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtoto Yesu ili alete Mvua ya kutosha isiyokuwa na madhara,kwani mpaka sasa Mkoa wa Dodoma na Kanda ya kati kwa ujumla bado haina mvua,"amesema Askofu huyo.


Pamoja na hayo amesema na wakristu wanapaswa kutumia kipindi hiki kujifungamanisha na maombi pia kwa Mtoto Yesu ambaye hashindwi na lolote aweze kuliepushe taifa dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO-19,na hasa maambukizi mapya ya sasa yanasambazwa na Kirusi cha Omicron.


Hata hivyo Mchungaji huyo Mkuu wa Jimbo ametumia nafasi hiyo kwa kusema "Nawaonya pia Vijana wanaotumia madawa ya kulevya kuacha mara moja  tabia hiyo,madhara yake ni kuwaharibia maisha yao wenyewe na kupunguza nguvu kazi ya familia na Taifa lote kwa ujumla,ili kuondokana na yote haya lazima tukubaki kumshirikisha Mwenyezi Mungu,"amesisitiza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com