Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MCHUNGAJI NA MKEWE WAKAMATWA KWA KUSHIRIKI KUMBAKA BINTI


JESHI la Polisi Jimbo la Ogun linasema kuwa limemkamata mchungaji mmoja kwa tuhuma za kula njama na mkewe kumbaka msichana wa miaka 16.

Taarifa kutoka kwa kikosi hicho cha polisi nchini Nigeria ilisema Mchungaji Peter Taiwo alikamatwa tangu Ijumaa katika Kanisa la Christ Apostolic Bible Church huko Alaja Oke, Abeokuta.


Polisi wanasema mkewe, Elizabeth, pia alikamatwa kwa tuhuma za kula njama ya ubakaji. Aidha, polisi wanasema waliwakamata watuhumiwa hao baada ya msichana huyo kuwalalamikia kuhusu tukio hilo.


Msichana huyo alieleza kuwa alipokwenda kanisani katika mazoezi ya kwaya, mke wa mchungaji alimpigia simu na kumwambia aende kwenye chumba ambacho mchungaji huyo alikuwa akimtafuta kwani atampeleka. 

Aliingia chumbani na mchungaji akafunga mlango na kutumia nguvu kukidhi mahitaji yake.


Alieleza kuwa baada ya mchungaji huyo kumaliza alichokuwa akifanya, mkewe aliingia chumbani humo na kumkuta akilia na kumsihi aache kulia na kumwambia kuwa sasa yeye ni mwanamke huku akimwonya kuwa asithubutu kusema yaliyotokea.


Aliambiwa kuwa iwapo atamwambia mtu yeyote basi atakufa.

 Polisi wanasema bado wanaendelea na uchunguzi na watawafikisha washukiwa hao mahakamani.

 Hata hivyo washukiwa hao tayari wamekiri mashtaka hayo ya ubakaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com