Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia kijana mmoja mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa kijiji cha Kinyasi kati wilayani Kondoa Mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 75.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 22, 2021 jijini Dodoma kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amesema kuwa kijana huyo alimbaka mama yake kwa kumvamia wakati amelala na mtuhumiwa wa tukio hilo bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Chanzo - Wasafi FM
Social Plugin