Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HII NDIYO TV AMBAYO UNAWEZA KULAMBA KIOO CHAKE 'SKRINI' KUONJA LADHA YA CHAKULA


Namna ambavyo unaweza kulamba TV hiyo


Mfano wa skrini ya TV "unayoweza kulamba" ambayo inaweza kuwa na ladha ya chakula imetengenezwa na profesa wa Kijapani, Reuters inaripoti.


Katika teknolojia hiyo Inayojulikana kama Taste-the-TV, makopo kumi yananyunyizia ladha kwenye "hygienic film"(filamu ya usafi) ambayo inakunjwa juu ya skrini ili mtazamaji ailambe.


Profesa Homei Miyashita wa Chuo Kikuu cha Meiji, alisema kuwa TV ya aina hiyo inaweza kutumika kutoa mafunzo kwa wapishi au wahudumu wa mvinyo.


Iwapo itatengenezwa kibiashara, TV hiyo itagharimu $875 (£735), alikadiria.

"Lengo ni kufanya iwezekane kwa watu kukifahamu kitu kama kula kwenye mgahawa upande mwingine wa dunia, hata wakiwa nyumbani," aliiambia Reuters.

Anaripotiwa kuwa katika mazungumzo na watengenezaji kuhusu matumizi mengine ya teknolojia ya kunyunyizia ladha, kama vile kuongeza ladha kwenye mkate.


Profesa anatazamia kujikita katika ulimwengu wa "maudhui ya ladha" ya kupakuliwa (downloadable).


Katika enzi hii ya Covid-19, aina hii ya teknolojia inaweza kuboresha jinsi watu wanavyoungana na ulimwengu wa nje, Prof Miyashita anaamini.


Lakini kwenye Twitter watu walishangaa ikiwa katikati ya janga la ulimwengu ulikuwa wakati sahihi wa kuzindua Taste-the-TV.


"Wakati wa janga hili?" aliandika mmoja, "Kuna uwezekano mkubwa wa kufanya kufanikiwa katika nyakati za corona :)" mwingine alitania.

Hapo awali, Prof Miyashita na wanafunzi wake walitengeneza vifaa mbalimbali vinavyohusiana na ladha, ikiwa ni pamoja na "uma unaofanya chakula kuwa na ladha zaidi".


Waandishi wa habari wakioneshwa onyesho la kifaa hicho na mwanafunzi.

Aliiambia mashine kuwa alitaka "chokoleti tamu", na baada ya majaribio machache agizo lilinyunyiziwa kwenye filamu ya plastiki ili aionje. "Ni kama chokoleti ya maziwa," anaripotiwa kusema.

Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com