Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mshambuliaji wa Paris Sanit-Germain (@psg) Lionel Messi (@leomessi) kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia “Ballon d’Or” kwa mara ya 7, hivi karibuni nyota huyo ameamrishwa na mahakama nchini Hispania kubomoa hoteli yake ya kifahari iliyopo katika jiji la Barcelona kutokana na kutokidhi viwango vinavyohitajika.
Messi alinunua jengo hilo mwaka 2017, ambapo lina jumla ya vyumba 77 vya kulala, kwa thamani ya Euro Milioni 30 (sawa na Tsh Bililioni 77.76), ambapo hata hivyo inaelezwa kuwa mamlaka nchini humo ilikuwa tayari imeshaidhinisha ubomoaji wa jengo hilo hata kabla ya Messi kulinunua.
Mpaka sasa Muargentina huyo anatarajiwa kutuma mawakili wake kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya mahakama na kujaribu kutafuta mbinu mwafaka ya kumaliza utata huo bila ya kupoteza mali yake.
Social Plugin