Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dr. Alex Malasusa kufuatia kifo cha baba yake mzazi, Mchungaji Gehaz Japhet Malasusa.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo hicho na kutoa salamu za pole kwa familia ya askofu huyo, ndugu, jamaa na marafiki na kumuombea kwa Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
Mzee Malasusa alifariki dunia usiku wa kuamkia Desemba 8, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu.
Social Plugin