Steven Yamba(44) mfanyabiashara wa nchini Zambia ameripotiwa kumshushia kipigo kikali mke wake wa ndoa Kangwa Mwango(33) na kufariki asubuhi saa tatu Desemba 25 siku ya Krismasi.
Mwanaume huyo alijaribu kumpeleka mkewe hosptali lakini alipogundua mkewe kafariki na yeye aliamua kukimbilia dukani kununua dawa ya kuulia wadudu akanywa na yeye kufariki dunia.
Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wamesema uchunguzi wa awali umeonesha mfanyabiashara huyo usiku wa saa moja katika mkesha Krismasi ndiyo alianza kumpiga mkewe hadi asubuhi na mke huyo alipoanza kuwa hoi ndio akajifanya kutaka kumpeleka hospitali ambapo alifariki dunia.
Social Plugin