Picha ya kushangaza na maneno yake yalinikumbusha hadithi ya jamii zilizotishwa na mawimbi ya mchoro wa kutisha wa Jan Asselijn, "The Breach of the Saint Anthony's Dike karibu na Amsterdam."
Mchoro huo unaunda upya janga la wimbi ambalo lilipiga pwani ya Uholanzi mapema asubuhi ya Machi 5, 1651.
2. Sanamu, Italia, 2021
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Tweet iliyotafuta (kwa kejeli) kuelewa asili ya vipimo vya haraka vya covid ilienea kwenye mitandao ya kijamii mnamo Novemba.
Chapisho linaonyesha kikundi cha sanamu ya Villa ya Tiberius ya karne ya kwanza huko Sperlonga nchini Italia, inayoonyesha kupofushwa kwa Cyclops Polyphemus.
Kulingana na hadithi, Ulysses hatimaye ataweza kudhibiti Polyphemus (ambaye alikuwa amekula wanandoa kadhaa kutoka kwa wasaidizi wa shujaa wa epic) kabla ya kutoboa jicho lake moja na mkuki mkali.
3. Ndege ya jeshi la wanahewa la Marekani, Uwanja wa Kabul, Agosti 2021
Wakati kundi la Taliban lilipoingia katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, tarehe 15 Agosti, ndege ya Jeshi la Wanahewa la Marekani iliyokuwa ikielekea Qatar ikawa tumaini la mwisho la kuuhamisha mji huo kwa Waafghanistan wengi.
Picha za mamia ya watu waliokata tamaa kwenye ndege ya C-17 Globemaster III ni miongoni mwa picha za kushangaza zaidi zilizonaswa mwaka huu.
Umati wa watu (unaokadiriwa kuwa kati ya watu wazima na watoto 640 hadi 830) unaweza kulinganishwa na maono ya sanamu ya hivi majuzi " Angels Unawares" ya msanii raia wa Canada Timothy Schmalz - meli ya shaba ya urefu wa mita 6 iliyojaa roho zilizohamishwa.
4. Wanaanga, Israel, 2021
Wanaanga wawili wakitembea wakiwa wamevalia mavazi ya safari za anga za mbali wakati wa mafunzo ya kwenda sayari ya Mars kwenye bonde la Ramon katika jangwa la Negev nchini Israel.
Eneo hii lilitumiwa kwa mazoezi ya wanaanga sita kutoka Austria, Ujerumani, Israel, Uholanzi, Ureno na Uhispania, kwa sababu ni mfano wa hali ambazo watakabiliana nazo kwenye sayari ya Mars.
Picha hazikuonekana kuonyesha mahali katika ulimwengu wetu, lakini mandhari ya upweke kama yale yaliyowazwa na msanii wa Ufaransa Yves Tanguy.
5. Waandamanaji, Scotland, Novemba 2021
Wakati wa mkutano wa COP26 Novemba, wanaharakati kutoka kundi la Ocean Rebellion waliandamana mbele ya viwanda vya kusafisha mafuta na vituo vya kemikali za petroli huko Grangemouth, Scotland.
Wakijiita "Vichwa vya Mafuta," waandamanaji hao walitumia mitungi ya plastiki au mapipa kubebea petroli kama maski huku wakitema mafuta na kurusha pesa bandia kukejeli tabia ya wawekezaji na wanasiasa ambao wanadai wanachukua hatua pole pole katika ahadi zao za kukomesha ukataji miti ifikapo 2030.
Picha yenye ufanisi wa kuona inakumbusha 'leitmotif' katika kazi za sanaa za wasanii wa kisasa ambayo huvutia umakini kwa athari za mwanadamu kwa mazingira.
6. Mpiga mbizi, China, Januari 2021
Mnamo Januari, mwanamke alipigwa picha akipiga mbizi kutoka kwenye jiwe la barafu hadi kwenye ziwa lililoganda huko Shenyang, mkoa wa Liaoning kaskazini mashariki mwa China.
Katika picha, yeye anabaki kusimamishwa milele. Mwili wake unaambatana na sehemu iliyopimwa ya barabara yenye theluji.
Ukali wa mazingira unaomngojea muogeleaji humfanya aanguke kwa njia isiyoeleweka kama tukio ambalo msanii wa Ufaransa Yves Klein alidai kulifanya kutoka dirisha la Paris mnamo 1960 aliloliita (Leap into the void).
7. Msichana, Gaza, Mei 2021
Kwenye mzozo mbaya zaidi kati ya Israel na Palestina tangu 2014, mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel kujibu mashambulizi roketi kutoka kundi la Hamas, yaliharibu nyumba ya msichana huko Beit Hanoun, Gaza, Mei 24.
Picha ya msichana huyo, akiwa hana viatu kwenye kifusi, akitazama upeo wa macho yake inahuzunisha.
8. Ziwa, Serbia, 2021
Picha ya taka kwenye barafu inayoziba mto Lim karibu na mji wa Priboj nchini Serbia inashangaza.
Picha hii ya taka katika mazingira safi inakumbusha maono ya msanii wa Cuba Tomás Sánchez, ambaye aligundua upya mahali pa kusulubiwa kwa Kristo nje ya Yerusalemu katika mchoro wake wa 1994, "Kusini mwa Kalvari."
Mchoro wa Sánchez unaeleza kwamba wokovu ni kazi nyingi ya kimwili kupitia matope ya kawaida na vile ni safari ngumu ya kiroho.
9. Mtoto, Indonesia, 2021
Mvulana mwenye umri wa miaka 8 anaomba katika mitaa ya Depok, Indonesia. Ngozi yake imefunikwa na mchanganyiko wa rangi na mafuta ya kupikia .
Aldi ni sehemu ya kikundi kinachojulikana kama "Manusia Silver" ambao hutumia mbinu hii hatari kuvutia wasaidizi
Picha yake katikati ya mwa msongamano wa magari inasikitisha.
10. Maandamano Bungeni, Marekani, Januari 2021
Picha za wafuasi wa Donald Trump wakipambana vikali na polisi wa Bunge la Marekani mnamo Januari 6 zilishtua ulimwengu.
Wavamizi waliokuwa wakimuunga mkonoTrump walikuwa wakipinga kuidhiniswa kwa Joe Biden kama rais mteule wa Marekani.
Inaweza kushangaza wengine kwamba taswira ya Wamarekani wakipigana ni sehemu ya sanamu za eneo hilo
11. Meli ya mizigo ya Ever Given, Misri, Machi 2021
Wakati meli kubwa ya mizigo ilipokwama kwenye mfereji wa Suez nchini Misri Machi 2021, usafiri wa meli duniani ulisimama.
Ikisafiri kutoka Uchina kwenda Uholanzi, meli ya Ever Given ilikuwa imebeba kontena 20,000 wakati ilikwama karibu na mwisho wa mfereji mnamo Machi 23.
Picha za tingatinga dogo lililojaribu kuikomboa meli hiyo kubwa ziliibua matukio mengi ambayo kwa upande wake yanakumbusha picha maarufu na za kejeli..
12. Mtoto, Kenya, 2021
Mnamo Novemba, washindi wa shindano la Wapiga Picha wa Mazingira wa mwaka 2021 walitangazwa.
Katika kitengo cha Hali ya Hewa, picha ya mvulana aliyevaa maski ya oksijeni na kushikanisha na kipumuaji, ambacho nguvu yake ni mmea uliopandwa karibu naye, ilitambuliwa.
Ni maelezo yenye nguvu ya matokeo ya uharibifu wa mazingira. Picha ya Kevin Onyango ya "The Last Breath" ilichikuliwa jijini Nairobi, Kenya.
Picha haionekani tu kuelezea mustakabali wetu usio na uhakika, bali pia katika historia ya sanaa, yenye kazi zenye ushawishi kutoka zamani.
13. Mchoro, Ufaransa, Oktoba 2021
Picha ya wazima moto wa Ufaransa wakiinua blanketi la zima moto ili kulinda moja ya hazina nyingi za Kanisa Kuu la Saint-Andre wakati wa mazoezi ya moto huko Bordeaux, Ufaransa, mnamo Oktoba, yenyewe ni kazi ya sanaa.
Mchoro huo uliundwa na Jacob Jordaens karne ya 17 na unaonyesha Kristo aliyesulubishwa anayekufa akijeruhiwa kwa mikuki mirefu katika giza nene linalozidi kuongezeka.
Ngazi kwenye pande zimeunganishwa na magogo ya kupanda na kushuka yaliyoonyeshwa kwenye uchoraji, na kubadilisha kazi kuwa maono ambayo si ya kweli kabisa au ya kufikiria.
Kumbukumbu hii hutuunganisha na siku za nyuma na mila ya kazi nyingi ambazo viwango vyake vya maana hupimwa pamoja na ngazi za kupanda.
14. Watoto, Ethiopia, Julai 2021
Mwezi Julai, picha ilionyesha kundi la watoto wakiwa wamesimama chini ya mti wakiwa wamefunikwa na ukungu katika eneo la kambi ya wakimbizi ya Eritrea ya siku zijazo karibu na kijiji cha Dabat, kaskazini mashariki mwa jiji la Gondar nchini Ethiopia.
15. Wahudumu wa afya, India, Octoba 2021
Ili kusherehekea kipimo cha bilioni moja cha chanjo ya covid nchini India, wahudumu wanne wa wauguzi katika Hospitali ya Ramaiah huko Bangalore walipiga picha mwezi wa Oktoba wakimwiga mungu wa kike Durga, ambaye kwa kawaida anaonyeshwa akiwa na mikono mingi, kila mmoja uiwa na silaha na ambaye huwashinda kwa ustadi. adui zake.
Sio mara ya kwanza kwa Durga, mungu muhimu wa Kihindu aliyepewa sifa ya kupigana na nguvu za uovu, ametumiwa wakati wa janga hi
Mnamo Oktoba 2020, picha za sanamu ya mita mbili ya Durga, ambayo msanii wa India Sanjib Basak alikuwa ameunda kwa kutumia sindano za kutupwa na malengelenge ya vipande vya dawa vilivyoisha muda wake, zilikuwa vimeenea.
Sanamu ya Basak iliishia kuwa kazi ya matumaini katika uso wa uchungu na shida.lo.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin