Mkazi wa eneo la Bible Mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa, Doricas Richard mwenye umri wa miaka 23 anauguza majeraha baada ya mumewe kudaiwa kumkata masikio kufuatia ugomvi na wivu wa mapenzi.
Imeelezwa kuwa, mume wa Doricas alianza kuhisi kama mkewe huyo ana hawara baada ya kufuatilia mazungumzo kwenye simu ya mwanamke huyo kwa muda mrefu.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana baada ya mume huyo kuingia ndani na kutaka simu ya mkewe huku akimtamkia kuwa anataka masikio ili kumkomesha, hivyo alimkata masikio yake kwa kisu kisha kutokomea kusikojulikana.
Via - Global Publishers
Social Plugin