Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBWA KOKO AVAMIA DUKA LA DAWA, ASHAMBULIA WAHUDUMU


Kizaazaa kimeshuhudiwa mjini Thika nchini Kenya baada ya mbwa koko kuruka kwenye duka la dawa, maarufu Chemist kuvamia na kuwashambulia wahudumu ghafla.

Kisa hicho kilifanyika Disemba 24,2021 katika duka la Menya Chemist wakati ambapo wahudumu walikuwa kwenye shughuli zao za kila siku. 

Wakazi walisema ilikuwa kama filamu kwenye duka hilo huku wahudumu wakilia na kuomba usaidizi kumkabili mbwa huyo.

"Sisi tumeona maajabu hapa. Hii ni umbwa sijui imetoka wapi? Imeingia hapa na kuanza kuvamia watu. Imebidi tuiue," alisema mmoja wa wakazi.

 Wakazi walisema kilikuwa kisa cha kushangaza na hawakujua sababu ya kuchagua duka hilo na kushambulia wahudumu.

 "Tunashangaa sana kuhusu kisa hiki. Hii umbwa imeacha watu wengi, imepitana na hata magari lakini ikakuja tu hapa na kumuuma huyo," mkaazi mwingine alisema.

Inaarifiwa mbwa huyo aliuma kidole cha mwathiriwa hadi kukikata na kisha akakitema na kulala ndani ya duka.

Wakazi wenye hamaki waliamshambulia na kumpa kichapo hadi kufariki dunia na kuchukuliwa na maafisa wa kanjo.

 Ilibidi mwathiriwa kukimbizwa katika hospitali kupokea matibabu baada ya kupoteza kidole chake cha gumba. 

John Ngumba, mwenyekiti wa wafanyibiashara mjini Thika, alisema watahakikisha kuwa mwenye mbwa huyo atashtakiwa.

 MCA wa Wadi ya Thika Andrew Kimani alikosoa mmiliki wa mbwa huyo kwa kumwachilia aranderande na kuhatarisha maisha ya wakazi. 

Aliahidi kuhakikisha kuwa wote walioshambuliwa na mbwa huyo wamepata matibabu yanayofaa na mmiliki wa mbwa huyo kuwajibika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com