RAIS MWINYI AWAAPISHA WAJUMBE WAPYA WA TUME YA MIPANGO



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Wajumbe wapya wa Tume ya Mipango ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, kuwa Mjumbe mpya wa Tume ya Mipango, hafla hiyo imefanyika leo Desemba 27,2021, katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mwanasheria Mkuu, Mhe.Dkt. Mwinyi Talib Haji, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.


Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu jijini Zanzibar ikiwa ni kikao cha kwanza cha tume hiyo katika Awamu ya Nane ya uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah walishiriki ikiwa ni Wajumbe kutokana na vyeo vyao.


Mara baada ya kiapo hicho, Rais Dkt. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wajumbe hao wapya aliowaapisha pamoja na wale wa zamani wanaoendelea.


Katika pongezi hizo, Rais Dkt. Mwinyi alieleza matumaini yake makubwa kwa wajumbe hao wa Tume ya Mipango ya Zanzibar katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar,Mhe Jamal Kassim Ali,kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango,hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya Kiapo ya Waziri wa Ardhi, Maendeleo na Makazi Zanzibar, Mhe.Riziki Pembe Juma, baada ya kumuapisha kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe Mudrik Ramadhani Soraga, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaban, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.




Wajumbe walioapishwa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Riziki Pembe Juma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga.


Wengine ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban,Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Suleiman Masoud Makame,Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Lela Muhamed Mussa, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Abdalla Hussein Kombo pamoja na Dk. Rahma Salim Mahfoudh Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Zanzibar, Mhe. Rahma Kassim Ali, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe.Lela Mohammed Mussa, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Uchumu wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Abdalla Hussein Kombo,kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dk. Rahma Salim Mahfoudh kuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar. (Picha zote na Ikulu).


Wajumbe hao wapya walioapishwa leo wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa maslahi na uchumi wa Zanzibar.

Nao wajumbe wa zamani wa Tume hiyo ya Mipango ya Zanzibar Mohammed Faki Mohammed pamoja na Profesa Semboja Haji Hatib walitoa shukurani zao kwa Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kwa kuendelea kuwaamini kuwa Wajumbe wa Tume hiyo na kuahidi kwamba wataendelea kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post