Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishana msaidizi Henry Mwaibambe amesema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Leonard Morisha alifariki tarehe 27 mwezi wa 6 mwaka 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo ,na kushangaza watu kwa kuonekana tena katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama Oktoba 2020 na wazazi wake wakampata na kumtambua Tarehe 12 Desemba mwaka huu.
Katika maelezo yake, Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo alifahamika kwa jina la Tereza Lusolela miaka (48) alithibitisha kuwa kuwa huyo ni mwanaye na baada ya jeshi la polisi kufukua kaburi hakukutwa sanduku wala vipande vya kanga ambavyo mama amedai walimzikia mwanae miaka 4 iliyopita
Sambamba na hilo ACP Henry Mwaibambe ameziomba hospitali kubwa kumsaidia kimatibabu mtoto huyo kwa sasa haongei baada ya kuonekana hai huku Ulimi wake ukiwa Umekatwa.
Inaelezwa kuwa katika hali isiyo ya kawaida Mtoto mmoja ambaye amefahamika kwa jina Leonard Morisha (11) mkazi wa Kijiji cha Ngemo, wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, aliyefariki dunia katika hospitali ya wilaya ya Geita na kuzikwa Juni 27, 2017, anadaiwa kufufuka baada ya Oktoba 2020 kuonekana wilayani Kahama na wazazi wake wamempata akiwa amekatwa mishipa ya sehemu ya ulimi na kupoteza uwezo wa kuongea.
Social Plugin