Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MSANII MUSOMA AACHIA WIMBO MPYA 'MALALAMIKO'... TAZAMA HAPA


Msanii Musoma

Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 blog, Dodoma

MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya Giraruma Yusuphu Kisheri maarufu kwa jina la Musoma ameachia wimbo uitwao Malalamiko ambao amemshirikisha Msanii mwenzake Coclyn huku akihidi kuendelea kutoa nyimbo zenye ujumbe na zinazowakonga watanzania.


Musoma ambaye anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo Umenichota aliomshikirisha Staa wa Bongo Star Search,Mesha Mazing,Miss Dom aliomshirikisha One Six na Njoo njoo na Zamu yetu.

Akizungumza na Malunde blog Desemba 1,2021,Msanii huyo ambaye ni mwalimu wa shule ya Msingi Amani ya Jijini Dodoma amesema wimbo wa Malalamiko umekuja kueleza kwa kina kuhusu usaliti ambao umekuwa ukitokea katika jamii.

Musoma amesema matarajio yake ni kuendelea kutoa nyimbo zenye kuelimisha,kuburudisha na kuonya jamii juu ya mambo mbalimbali huku akisisitiza watanzania wazidi kumuunga mkono.

Katika hatua nyingine, Msanii huyo amesema anatarajia hivi katibuni kutoa wimbo uitwao Yatima ambapo amedai atamshirikisha Msanii mwenye jina kubwa hapa nchini Linex.

Tazama Hapa Video : MUSOMA FEAT.COCLYN - MALALAMIKO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com