Mwanamke mmoja askari amekamatwa nchini Nigeria kwa kukubali ombi la kuolewa akiwa kazini, msemaji wa jeshi amesema.
Alikuwa amekiuka kanuni za maadili za kijeshi kwa "kujiingiza katika mapenzi akiwa amevalia magwanda rasmi ya jeshi", aliongeza.
Video iliibuka wiki iliyopita ya askari huyo akipokea pete kutoka kwa mwanaume aliyepiga magoti mbele yake, huku watazamaji wakishiriki furaha yao.
Kundi la kutetea haki za wanawake limeshutumu jeshi kwa kumbagua.
Wanadai Kuwa Hatua kama hiyo haikuwa imechukuliwa dhidi ya wanajeshi wa kiume waliohusika "katika maonesho ya hadharani ya mahusiano ya kimahaba wakiwa wamevalia sare kamili za kijeshi", kikundi cha Women Empowerment and Legal Aid.
Mwanaharakati wa haki za binadamu na aliyekuwa mgombea urais wa Nigeria Omoyele Sowore alilaani uamuzi wa jeshi na kuuita "udhalilishaji".Afisa huyu anatuhumiwa kukiuka kanuni za maadili za kijeshi kwa "kujiingiza katika mapenzi akiwa amevalia sare za jeshi la Nigeria",Video ilisambaa mitandaoni wiki iliyopita ya askari huyo akipokea pete kutoka kwa mwanaume aliyepiga magoti mbele yake, huku watazamaji wakishiriki furaha ya wapenzi hao.
Mwisho wa Instagram ujumbe, 1
Mwanajeshi huyo alikuwa amekubali pendekezo la ndoa kutoka kwa mwanafunzi katika mpango wa mafunzo kwa vijana wa serikali, unaojulikana kama Kikosi cha Huduma ya Vijana kwa Kitaifa (NYSC).
Kama sehemu ya mpango wa lazima wa mwaka mzima kwa wahitimu kutoka vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu ya juu hupata maagizo kutoka kwa jeshi.
Pendekezo hilo la ndoa lilitolewa wakati wa programu ya mafunzo katika jimbo la Kwara magharibi.
Haijulikani tukio hilo lilifanyika lini, lakini video yake ilisambaa wiki iliyopita.
Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii waliwapongeza wanandoa hao, na kumsifu mwanaume huyo kwa kumchumbia. Wengine walimtania askari huyo.
Msemaji wa jeshi Jenerali Clement Nwachukwu aliiambia BBC kwamba mwanajeshi huyo alikiuka maadili ya jeshi, na pia sera yake ya mitandao ya kijamii.
"Matendo yake yalikuwa yanazuia utaratibu mzuri na nidhamu ya kijeshi
"Kazi [ya wakufunzi] ilikuwa kuwafundisha wanachama wa kikosi cha vijana na kutojiingiza katika uhusiano wa kimahaba na yeyote kati yao," Jenerali Nwachukwu aliongeza.
NYSC bado haijatoa maoni.
Chanzo - BBC Swahili
Social Plugin