Mfano wa nyaya za umeme
Na John Walter-Babati
Watu wasiofahamika wamevamia nyumba ya mchungaji na kuiba nyaya za umeme na kuharibu mfumo mzima wa umeme (wire ring) uliokuwa umewekwa katika nyumba hiyo katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Komoto mjini Babati.
Nyumba hiyo ya Mchungaji ipo katika hatua za mwisho za umaliziaji kabla ya mchungaji kuhamia.
Hayo yamebainishwa na Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo usharika wa Komoto Mchungaji Godlsten Mkenda katika ibada iliyofanyika jana Jumapili Desemba 12 kanisani hapo.
Kutokana na tukio hilo kiongozi Mchungaji Godlsten Mkenda ameongoza maombi maalum yaliyofanywa na waumini wa kanisa hilo kuwaombea kwa Mungu waliotenda uhalifu huo wa kutwaa mali isiyo yao ili waokoke na kumrudia Mungu.
Hata hivyo mchungaji Mkenda aliwataka waumini watoe taarifa pindi wanapopata taarifa za waliohusika na tukio hilo.
Mchungaji Mkenda amesema "Katika Roho ya Kikristo, tunaomba kila mmoja aliyehusika kuguswa na Roho Mtakatifu na kurudisha nyaya hizo"