Nyoka huyo hatari alionekana katika upande wa dereva
Miongoni mwa nyoka hatari zaidi duniani amepatikana huko Salford baada ya kunusurika safari ya maili 4,000 katika shehena ya meli kutoka Pakistan.
Nyoka huyo aligunduliwa kwenye kontena la matofali, ambalo lilikabidhiwa kwa mtaalamu wa matofali wa Manchester mwezi uliopita.
Mkaguzi wa RSPCA, Ryan King aliitwa ili kumuokoa nyoka huyo mwenye sumu
Alisema aligundua kwa haraka kuwa nyoka huyo "alikuwa na uwezo zaidi wa kuua watu kwa sumu yake yenye sumu kali."
"Wakati mwingine tunapata kazi kama hizi na inageuka kuwa nyoka asiye na madhara," alisema.
"Tumehudhuria hata ripoti za nyoka ambazo zinageuka kuwa vifaa vya kuchezea vya plastiki."
Bw King alisema mara moja alitambua baada ya "kumtazama kwa haraka" jinsi nyoka huyo alivyokuwa na sumu
Mkaguzi RSPCA Ryan King alisema ni heshima kubwa kwake kukabiliana na nyoka wa aina ile"
Dereva wa forklift katika kampuni hiyo kwenye Barabara ya Langley alimpata nyoka huyo siku ya Ijumaa.
Meneja wa vifaa Michael Regan alimfungia nyoka huyo kwenye sanduku na kuripoti suala hilo kwa RSPCA.
"Nilijua kujiweka mbali lakini bila shaka sikujua jinsi nyoka huyu alivyokuwa mbaya - nilishtuka sana," alisema.
Nyoka huyo anayepatikana zaidi barani Asia, amehamishiwa kwenye kituo chenye leseni maalum ya kuhudumia wanyama watambaao wenye sumu kali.
Nchini India, ambapo karibu nusu ya vifo vya kung'atwa na nyoka duniani kote vinavyodhaniwa kutokea, nyoka ni mojawapo ya spishi nne ambazo kwa pamoja zinachangia idadi kubwa zaidi ya vifo vya binadamu, RSPCA ilisema.
Bw King alisema ni jambo la kustaajabisha kwamba nyoka huyo alinusurika katika safari hiyo na kuweza kuishi kwa wiki kadhaa katika hali ya baridi kama hiyo.
"Ni wadogo sana na angeweza kumng'ata mtu kirahisi na inaonekana amekuwa kwenye eneo la ujenzi wa matofali kwa takriban mwezi mmoja," alisema.
"Kinga ya sumu ya nyoka huyo huwa inapatikana katika nchi ambako nyoka anatoka lakini ana sumu kali sana- ni ngumu kwa muathirika kuokolewa."
Chanzo : BBC SWAHILI