POLISI DODOMA WAZUNGUMZIA TUKIO LA WASIOJULIKANA KUVUNJA NYUMBA YA MBUNGE HUMPHREY POLEPOLE

 

Humphrey Polepole
*

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma, limesema lianendelea na uchunguzi pamoja na msako kuwabaini waliovamia nyumba ya Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. Humprey Polepole na kuiba baadhi ya vitu ndani ya nyumba hiyo.

Akitoa ufafanuzi huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga amesema; “Jana Desemba 12, 2021 majira ya saa tatu na nusu katika mtaa wa Mabuba jijini Dodoma Polepole alibaini kuvunjiwa dirisha la nyumba anayoishi na kuibiwa televisheni moja ya flat screen inchi 55 na spika moja ya bluetooth, ambazo thamani ya mali zote hizo bado haijafahamika.


“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mhe. Mbunge Humphrey Polepole alisafiri kwenda Mkoa wa Manyara katika shughuli zake, upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaendelea ili kuwatafuta wahusika wa tukio hilo na kuwachukulia hatua za kisheria.

“Suala la kwamba ni habari ya siasa sisi hatuoni kwasababu makazi yamevunjwa kwahiyo huwezi kusema wahalifu walikuwa wanamtafuta yeye, wangemkuta mwenyewe ishu ingekuwa tofauti ingekuwa ni unyang’anyi wa kutumia silaha au nguvu.


“Bado haieleweki ni lini hasa palivunjwa kwa hiyo si rahisi kujua kulikuwa na nia ya kutaka kumdhuru yeye kama yeye kwa sababu hakuna ujumbe wowote ambao tumeweza kuubaini kuwa umemtishia yeye maisha yake,” RPC wa Dodoma, Onesmo Lyanga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post