Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA 'RFA' WASHEREHEKEA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2022 NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM BUHANGIJA

Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA), Yusuph Magasha (kushoto) akikabidhi boksi la Taulo za kike kwa mmoja wa wanafunzi wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wafanyakazi wa Kituo cha Matangazo Radio Free Africa (R.F.A)  wamesherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2022 kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi ( ualbino), viziwi na watu wasioona wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA) waliofika katika kituo cha Buhangija leo Jumatano Desemba 2021, Yusuph Magasha amesema wameamua kusherehekea Sikukuu za mwisho wa mwaka 2021 na kufungua mwaka 2022 kwa kutoa zawadi kwa watoto hao.

Kwa niaba ya wafanyakazi wa Radio Free Africa,mimi na msafara huu tumekuja kukabidhi zawadi hizi ambazo tumechangishana sisi wafanyakazi wa Radio Free Africa pamoja na wadau wetu ili watoto wetu wafurahie sikukuu hizi za mwisho wa mwaka 2021 pamoja na kufungua vizuri mwaka mpya 2022”,ameeleza Magasha.


Amezitaja miongoni mwa zawadi hizo ni pamoja na Taulo za Kike ‘Pedi’, mchele,unga wa sembe, mafuta ya kupikia,maharage,sukari mafuta ya kujipaka, sabuni, dawa za meno,majani ya chai,madaftari,kalamu,juisi,pipi na biskuti.

Naomba mpokee hiki kidogo ambacho tumewaleteeni na tunaahidi kuendelea kuja hapa Buhangija ili kuwatelea mahitaji mbalimbali”,amesema.

Magasha ametumia fursa hiyo kuwaasa watoto hao kuzingatia masomo yao akiwasisitiza kuwa elimu ndiyo kila kitu katika maisha yao.

Akiwa katika kituo hicho mmoja wa watangazaji wa Radio Free Africa, Wambura Mtani ameahidi kuwa atakuwa anampatia mahitaji mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho cha Buhangija.

Kwa upande, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Msingi Buhangija Loyce Daudi amewashukuru wafanyakazi wa Radio Free Africa kutembelea kituo cha Buhangija na kuwapatia mahitaji mbalimbali huku akizitaja baadhi ya changamoto zilizopo kuwa ni Bili kubwa za maji zinazotokana na miundo mbinu chakavu ya maji pamoja na uhaba wa vifaa vya kujifunza na kujifunzia kwa wanafunzi hao.

Nao watoto wameeleza kufurahia ugeni wa waandishi wa habari na watangazaji wa Radio Free Africa, kuzungumza Mbashara 'Live' kupitia RFA na kuwashukuru kwa kuwapatia zawadi za Krismasi na Mwaka Mpya yakiwemo mahitaji ya vifaa vya shule yakiwemo madaftari na kalamu.

Miongoni mwa waandishi wa habari na watangazaji wa Radio Free Africa waliotembelea kituo cha Buhangija ni Wambura Mtani, Debora Mpagama, Emmanuel Mkuwi,Froza Mhando,Renatus Kiluvia, Pauline David, Nassoro Dimoso, Yusuph Magasha na dereva wao Andrew John.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA), Yusuph Magasha akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga leo Desemba 29,2021 wakati Wafanyakazi wa Kituo cha Matangazo Radio Free Africa walipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2022 kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto hao. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA), Yusuph Magasha akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga leo Desemba 29,2021
Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA), Yusuph Magasha akiwasisitiza watoto katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga kusoma kwa bidii.
Watangazaji wa Radio Free Africa (RFA) wakishusha mizigo yenye zawadi katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga leo Desemba 29,2021
Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA), Yusuph Magasha (kushoto) akikabidhi boksi la Taulo za kike kwa mmoja wa wanafunzi wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga
Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA), Yusuph Magasha (kushoto) akikabidhi madaftari kwa ajili ya wanafunzi katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga
Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA), Yusuph Magasha (kushoto) akionesha zawadi zilizotolewa na wafanyakazi wa Radio Free Africa kwa ajili ya wanafunzi wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya zawadi zilizotolewa na wafanyakazi wa Radio Free Africa (RFA),kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga leo Desemba 29,2021
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Msingi Buhangija Loyce Daudi akiwashukuru wafanyakazi wa Radio Free Africa kutembelea kituo cha Buhangija na kuwapatia mahitaji mbalimbali watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Mmoja wa watoto akiwashukuru wafanyakazi wa Radio Free Africa kutembelea kituo cha Buhangija na kuwapatia mahitaji mbalimbali 
Mmoja wa watoto akiwashukuru wafanyakazi wa Radio Free Africa kutembelea kituo cha Buhangija na kuwapatia mahitaji mbalimbali 
Mtangazaji wa Kipindi cha Show Time Radio Free Africa Renatus Kiluvia 'Bizzo Show Time' akimshikia simu mmoja wa watoto katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga akiongea Mbashara 'Live' kwenye kipindi cha Show Time
Mtangazaji wa Vipindi vya  Je Huu ni Uungwana?, Usiku wa Milenia na Lugha Gongana Radio Free Africa, Wambura Mtani akiwasisitiza watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga kusoma kwa bidii.
Mtangazaji wa Vipindi vya  Je Huu ni Uungwana?, Usiku wa Milenia na Lugha Gongana Radio Free Africa, Wambura Mtani akizungumza wakati akiomba kuwa mlezi wa mtoto anayelelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga ambapo ameahidi kuwa anampatia mahitaji mbalimbali.
Mtangazaji wa Vipindi vya Mkulima na UKIMWI na Jamii Radio Free Africa, Debora Mpagama akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Mwandishi wa Radio Free Africa Pauline David akigawa juisi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa Radio Free Africa wakigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa Radio Free Africa wakigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa Radio Free Africa wakigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa Radio Free Africa wakigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Mwandishi wa Radio Free Africa Pauline David akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Mtangazaji wa Radio Free Africa, Froza Mhando akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Mtangazaji wa Radio Free Africa Nassoro Dimoso akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Dereva wafanyakazi wa Radio Free Africa Andrew John akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Mtangazaji wa Radio Free Africa Emmanuel Mkuwi akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa Radio Free Africa wakipiga picha ya kumbukumbu na walimu walezi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa Radio Free Africa wakipiga picha ya kumbukumbu na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa Radio Free Africa wakipiga picha ya kumbukumbu na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com