Mkazi wa kijiji cha Masweya kata ya Mtunduru wilaya ya Ikungi mkoani Singida Vaileth Mtipa (32) amefariki dunia baada ya kupigwa na radi akiwa anazini (akichepuka) na mme wa mtu kwenye pagara.
Siku ya tukio Vaileth alikuwa na mpenzi wake Hassan Nzige na wakati wanafikwa na mkasa huo walikuwa wakishiriki mapenzi.
Inaelezwa kuwa radi ilipiga kabla mvua haijaanza kunyesha wakati huo wapendanao hao wakiwa kazini (wakifanya mapenzi) ambapo Nzige yeye alijeruhiwa wakati Vaileth alipoteza maisha.
Mwenyekiti wa kijiji cha Masweya Saidi Hongoa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
.
Social Plugin