Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SAMUEL ETO'O ACHAGULIWA KUWA RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA LA CAMEROON


Mchezaji Nyota wa zamani wa Cameroon Samuel Eto'o amechaguliwa kuwa rais wa shirikisho la soka la Cameroon (FecafootOfficie)

Eto'o, mwenye umri wa miaka 40, ameahidi mageuzi mbalimbali ili kustawi mchezo huo.

"Lazima tuwalete wanasoka katikati ya sera zetu," alisema baadaye. "Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba wale wanaocheza mpira huu wanapata maisha ya staha kutokana nayo."

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona, ​​Inter Milan na Chelsea pia ameahidi kujenga angalau viwanja 10 wakati wa uongozi wake.

"Nimezungumza na jumuiya ya wafanyabiashara na tuna uhakika tutapata wawekezaji wanaofaa ambao wanaweza kuandamana nasi katika kutimiza malengo yetu," Eto'o alisema kabla ya uchaguzi.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa Samuel Eto'o ataendesha soka la Cameroon kwa miaka minne ijayo baada ya kuchaguliwa kuwa mkuu wa shirikisho hilo siku ya Jumamosi.


Etoo ambaye aliwahi kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne alimshinda mpinzani wake Seidou Mbombo Njoya, makamu wa nne wa rais katika Shirikisho la Soka Afrika.


Wagombea saba walipaswa kushiriki uchaguzi, lakini watano kati yao walijiondoa asubuhi ya uchaguzi.
Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1



Kugombea kwa Eto'o kumeibua hisia za watu wengi kutokana na mkutano huo kutangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa ya Cameroon.


Sasa atakuwa mkuu wa FA ya Cameroon (Fecafoot) wakati nchi hiyo itaandaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari na Februari.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com