TAMASHA LA 'WOMEN GALLA' LA DIVINE FM LAFANYIKA KAHAMA... WAZIRI ATAKA WANAWAKE WABADILIKE KUKUZA UCHUMI

Rais wa sauti ya Wanawake wajasiriamali Nchini Bi Maida Waziri akitoa Elimu kwa Wanawake kupitia tamasha lililoandaliwa na kituo cha matangazo Divine Radio ( Women Galla).

Na Nyamiti Alphonce Nyamiti - Kahama
Pamoja na uwepo wa fursa nyingi za kiuchumi wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeelezwa kuwa wanawake wengi wameshindwa kuzitumia kwa baadhi yao kuwa na mifumo tegemezi kwenye uendeshaji wa maisha yao.

Yamebainishwa hayo na Rais wa sauti ya Wanawake wajasiriamali hapa Nchini Bi Maida Waziri wakati akitoa Elimu kwa Wanawake kupitia tamasha lililoandaliwa na kituo cha matangazo Divine Radio ( Women Galla).

"Mkoa huu unasifika kwakuwa na vyanzo vingi vya kiuchumi mmebarikiwa kuwa na Madini, Bandari ya nchi kavu, rasilimali watu na maeneo ya kufanyia kilimo badilikene mkuze uchumi wenu", alisema Waziri

Waziri ameitaka jamii ya wanaume kuendelea kuwapa fursa na kutoa kushirikiana kwa Wanawake kwakuwa wanauwezo mzuri wa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ametumia nafasi hiyo kuwataka Wanawake  wajasiriamali kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopa fedha hizo zinazotengwa na serikali kwa makundi ya vijana, Wanawake na walemavu.

"Sisi kama wilaya naomba nikuhakikishie Mgeni rasmi tumetenga 10% kwa kila halimashauri kutoa mikopo kwamakundi yote matatu tunazo halimashauri tatu" alisema Kiswaga

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Tamasha hilo wameitaka serikali kuwawekea mifumo mizuri ya upatikanaji wa Elimu ya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Rais wa sauti ya Wanawake wajasiriamali nchini Bi. Maida Waziri akisalimiana na akina mama kwenye tamasha lililoandaliwa na kituo cha matangazo Divine Radio ( Women Galla).
Wajasiriamali Kahama Wakijifunza  jambo kutoka kwa mkufunzi na muwakirishi wa Shirika la kazi Duniani bwana Benidict Mwampela..
Manager Wa Kituo cha Redio cha Divine Women Galla, Joshua Kasase akiwasalimia wana semina.
Raisi wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania.. Bi, Maida Waziri   Katikati akiwasili  ukumbi wa Miligo kwaajili ya semina ya akina mama Kahama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post