Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa majina ya Ravan Lazaro(48) mkazi wa Ludewa Mtaa wa Kanisani B mkoani Njombe amejinyonga kwa kutumia waya chanzo kikiwa ni kutotajwa katika misa ya shukrani kanisani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema mtu huyo na mkewe walikuwa na mtoto mwenye umri wa miaka 10 ambaye alivunjika mguu na baada ya kutibiwa hospitali na kupona walienda kanisani kutoa shukrani.
"Wakati wa shukrani padre wa kanisa alimtaja mama wa mtoto peke yake bila kumtaja baba hali iliyoleta sintofahamu na matokeo yake ameamua kujinyonga kwa kutumia waya," amesema Kamanda Issah.
Kamanda Issah amewataka viongozi wa dini kuzingatia umuhimu wa familia kwa kuwa inajumuisha baba na mama, akitajwa mmoja matokeo yake inaleta hali kama hiyo.
Social Plugin