Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ARSENAL YAMVUA UNAHODHA AUBAMEYANG KWA UTOVU WA NIDHAMU




KLABU YA ARSENAL imemvua unahodha Pierre-Emerick Aubameyang na hatacheza kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya West Ham kesho Jumatano usiku.

“Kufuatia ukiukaji wake wa nidhamu wiki iliyopita, Pierre-Emerick Aubameyang hatakuwa tena nahodha wa klabu yetu, na hatazingatiwa kwenye uchaguzi wa kikosi kitakacho cheza mechi ya Jumatano dhidi ya West Ham United.


“Tunatarajia wachezaji wetu wote, haswa nahodha wetu, kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na viwango ambavyo sote tumeweka na kukubaliana. Tunaangazia kikamilifu mechi ya kesho,” iliandika Arsenal.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com