Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ATUPWA JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 9




Mahakama ya wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha maisha jela George Lupindu (19) mkazi wa kijiji cha Ngalawale kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9.

Akisomewa hukumu hiyo na hakimu Isaack Ayengo katika shauri namba 37/2021 Geaorge Lupindu ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(3) cha Kanuni ya Adhabu, Sura namba 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyofanyiwa Mapitio mwaka 2019.

Imeelezwa na Mwendesha Mashtaka Asifiwe Asigile kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai 7 mwaka huu ambapo anadaiwa kumrubuni mtoto huyo (jina limehifadhiwa) wakati akitokea shuleni kwa kumdanganya kuwa anampeleka nyumbani kwao na kisha kumtenda unyama mtoto huyo.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com