Meneja Mipango ya Biashara wa Benki ya CRDB, Masele Msita (wa pili kulia)akipokea tuzo ya ubora kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Ubora barani Ulaya (ESOR), Edward Ryner katika hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika katika Hoteli ya Dusit Thani jijini Dubai, Falme za Kiarabu. Wengine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Falme za Kiarabu, Mohamed Mtonga (katikati), Meneja Mwandamizi Wawekezaji CRDB, Anna Mwasha (wa pili kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji wa Kijamii wa Benki hiyo, Joycelean Makele (kushoto) wakionyesha cheti cha mafanikio ya ubora.
========== ========== ==========
Mwaka 2021 unaisha vizuri kwa Benki ya CRDB ikiwa imetunukiwa tuzo tano ikiwamo ya ubora iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Taasisi ya Utafiti wa Ubora barani Ulaya (European Society for Quality Research-ESQR).
Benki hiyo imekuwa pekee ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kushinda tuzo kutoka taasisi hiyo inayoheshimika duniani kwa utafiti unaohusisha masuala ya ubora wa huduma na bidhaa. Akipokea tuzo hiyo katika Hoteli ya Dusit Thani jijini Dubai,Falme za Kiarabu, Meneja wa Mipango ya Biashara wa Benki ya CRDB. Masele Msita alisema ni heshima kubwa kwao kutambulika kwa ubora jambo linaloongeza imani kwa wateja na wadau wao wengine.
"Ubora ni sehemu ya uti wa mgongo wa benki yetu. Tunafurahi kupata tuzo hii kutoka ESQR inayoenda sambamba na matamanio yetu. Inathibitisha maono ya benki kubuni huduma bora na kuzifanya zipatikane kwa urahisi kwa wateja," alisema Msita.Meneja huyo alisema wakati wote benki ya CRDB inasisitiza na kuhamasisha ubora wa huduma na bidhaa inazotoa kwa wateja na wadau wengine inaoshirikiana nao katika ujenzi wa Taifa.
"Tunatimiza hili kwa kuimarisha mifumo yetu ya ndani," alisema msita kwenye hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyohudhuriwa na wawakilishi wa mashirika na kampuni zilizoshinda kutoka mataifa ya Afrika, Ulaya, Asia, Amerika na Australia.
Akiipongeza Benki ya CRDB kwa tuzo hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa ESQR, Edward Ryner alisema tuzo wanazotoa ni nembo ya uhakika wa ubora kwa wadau wa shirika au kampuni na huhamasisha menejimenti kuchukua hatua madhubuti kuendelea kuimarisha ubora kwa ajili ya wateja wake na wadau wengine.
Tuzo hii inaitambulisha Benki ya CRDB kuwa mzingatiaji mzuri wa maadili ya huduma kwa umaahiri mkubwa. Inaonyesha jinsi benki inavyojitofautisha sokoni kwa kubuni huduma salama za kidijitali,"alisema Ryner.
Tuzo hiyo inakuwa ya sita kwa Benki ya CRDB kushinda mwaka huu kwani ilishai buka mshindi wa kwanza wa tuzo ya uandaaji wa taarifa za fedha (FiRe)halafu ikawa benki bora ya tuzo za Bodi Taifa ya ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).
Tuzo nyingine ni benki bora yenye ubu-nifu Tanzania iliyotolewa na Jarida la Global Finance,benki bora inayokidhi matarajio ya wateja wake iliyotolewa na PANFinance pamoja na benki bora katika ubunifu wa kidijitali ya Consumer Choice Awards.
Benki ya CRDB ni miongoni mwa benki kubwa ya kizawa ambayo ina matawi nchini Burundi na inajipanga kufungua mengine katika Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC)pamoja na Sudan Kusini siku chache zijazo.
Social Plugin