Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA EQUITY NA NALA WASAINI MKATABA UTUMAJI WA FEDHA KIMATAIFA


Benki ya Equity kwa kushirikiana na kampuni ya kiteknolojia ya NALA, wamesaini mkataba wa utumaji fedha kimataifa utakaowasaidia watanzania wanaoishi nje ya nchi kutuma fedha kwa urahisi hapa nchini.

 Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Disemba 14, 2021 katika ofisi za benki ya Equity, mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Roberty Kiboti, amesema kupitia kampuni ya Nala watawarahisishia wanadiaspora kuwatumia ndugu zao fedha bila ya makato. Kiboti amesema kupitia huduma hiyo, serikali itapata fursa ya kupata mapato na kuzidi kuchochea kukua kwa uchumi wa nchi.

 “Leo tunazindua hudumaa hii,tumeona tuwasaidie wateja wetu wa diaspora kutuma pesa hapa nyumbani Tanzania na hii itasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia uwekezaji huu”, alisema Kiboti. Kadhalika Kiboti amesema kupitia makubaliano hayo wateja wa NALA wataweza kutuma fedha kupitia simu za mkononi na kuingia mojakwamoja katika akaunti ya benki ya Equity. Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Nala Benjamin Fernandes ameishukuru benki ya Equity pamoja na benki kuu ya Tanzania (BOT) kwa kukubali mfumo huo kutumika hapa nchini. Aidha amesema kampuni yao inaendeleza kutanua wigo ambapo mwakani wataingia katika nchi ya marekani ili wawafikie watanzania wanoishi huko.

 “Sisi ni kampuni ya kiteknolojia ambayo tumeanzisha bidhaa itakayowagusa watanzania kutuma pesa kutoka nje ya nchi kuja hapa, kwasasa takwimu zinaonesha kuna wanadiaspora zaidi ya 300,000 wanaoishi nchini uingereza ambao wanatumia hii huduma.

 tunatarajia mwakani tuingie nchini Marekani ili tuweze kuwapa huduma hii wanadiaspora wa huko”, alisema Fernandes.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com