Mzozo umezuka katika ukumbi wa bunge huko Ghana Jumatatu jioni wakati wabunge wakijadili mapendekezo ya kodi ya miamala ya kielektroniki ambayo yamegawa bunge kwa wiki kadhaa umepelekea Bunge kuahirishwa hadi Januari 18.
Ushuru wa asilimia 1.75, ambao utajumuisha ushuru wa malipo ya pesa kwa njia ya simu, ulipingwa vikali na upinzani tangu ulipopendekezwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita.
Wabunge walikimbilia mbele ya kitu cha Spika baada ya Naibu Spika Joseph Osei-Owusu kupendekeza ushuru huo kujadiliwa na kupigiwa kura chini ya utaratibu wa “dharura”.
Wengine walirusha ngumi na kugombana huku wengine wakiwazuia wenzao.
Social Plugin