Gabriel Boric ameahidi mageuzi makubwa ili kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kiuchumi nchini Chile
Mgombea wa mrengo wa kushoto Gabriel Boric ameshinda uchaguzi wa urais nchini Chile na kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Katika kile kilichotarajiwa kuwa kinyang'anyiro kikali, kiongozi huyo wa zamani wa waandamanaji mwenye umri wa miaka 35 alimshinda mpinzani wake wa mrengo mkali wa kulia José Antonio Kast kwa pointi 10.
Bw Boric aliwaambia wafuasi wake kuwa atajali demokrasia, na kuahidi mageuzi katika mfumo wa uchumi wa Chile.
Ataongoza nchi ambayo imetikiswa katika miaka ya hivi karibuni na maandamano makubwa ya kupinga ukosefu wa usawa na ufisadi.