IGP SIRRO ARUDI TENA KIBITI NA KUTOA MAAGIZO MAZITO KWA KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA
الخميس, ديسمبر 16, 2021
NA KIBITI, PWANI
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka viongozi wa dini pamoja na viongozi wa Kamati za Ulinzi na usalama za wilaya, tarafa, Vijiji na Vitongoji kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika suala zima la ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.
IGP Sirro amesema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kikazi Kibiti na Ikwiriri mkoani Pwani na kukutana na Viongozi wa Halmashauri tatu za Mkoa huo ikiwemo Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri pamoja na viongozi wengine wa Kamati za Usalama kwa lengo la kuwakumbusha wajibu wao.
Akizungumzia suala la usalama katika maeneo ya Kibiti na Ikwiriri IGP Sirro amesema kuwa, bado zipo changamoto chache kama wizi wa Pikipiki, mifugo na uhalifu mwingine mdogo mdogo ambao unaendelea kudhibitiwa.
Naye Diwani wa Kata ya Ikwiriri Ali Mbwana amesema kuwa, wananchi wanalipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha hali ya amani na usalama hasa eneo la Ikwiriri na Kibiti Inazidi kuimarika.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin