Kindi mmoja wa kijivu aliyewashambulia na kuwajeruhi watu 18 amekamatwa na kuuawa.
Mnyama huyo alijipatia jina la utani la Stripe baada ya uhusika mbaya katika filamu ya Gremlins.
Ilianza kushambulia watu huko Buckley, Flintshire, wiki iliyopita kwa muda wa siku mbili.
Hili lilikuwa ni tatizo kubwa kwa Corinne Reynolds, 65, ambaye alikuwa anamuhudumia kwa kumpa chakula tangu mwezi Machi anasema alikuwa mgeni wa mara kwa mara na alikuwa rafiki wa bustani yake.
Mwanzoni Stripe alikuwa anakuja kuiba chakula cha ndege na Bibi Reynolds alisema: "Miezi yote hiyo amekuwa sawa, hata angekuja na kuchukua karanga mkononi mwangu."
Lakini alisema alimng'ata wiki iliyopita alipokuwa akimlisha kwenye bustani yake, na kisha akaona ripoti za kuumwa na kushambuliwa kwa wengine kwenye ukurasa wa Facebook.
Aliongeza: "Baada ya kuona picha hizo zote za majeraha ya watu, niliwaza 'oh Mungu wangu, nini kimempata'?"
Bi Reynolds alisema alijua kwamba kuna kitu kinapaswa kufanywa na akafikiria "kwa sababu nilimjua, nilijua nina uwezo wa kumshika".
"Niliacha tu mtego karibu na eneo ninalomlisha kwa kawaida kwa dakika 20, na alikuwa ndani," aliongeza.
"Nilihisi aliniamini, na nikamsaliti."
Bi Reynolds aling'atwa kwenye kidole
Bi. Reynolds mara nyingi huchukua ndege waliojeruhiwa na kuwatunza mpaka wakipona na kuwaachia waende, alijielezea kuwa yeye ni mtu anayependa wanyama.
Alisema: "Bustani yangu ni kama hifadhi ya ndege. Lakini najua nilifanya jambo sahihi. Nina mjukuu wa miaka miwili, kama angeumwa kidole, angeweza kuacha."
Mwanamke anayeishi katika eneo moja aliripoti kushambuliwa alipokuwa akichukua masanduku ya taka , mwingine alisimulia kwenye mitandao ya kijamii jinsi alilazimika kwenda kuchomwa sindano alipong'atwa na kindi.
Kamanda wa Polisi alimchukua Kindi ambaye alikuwa amekamatwa nyumbani kwa Bi. Reynolds na, baada ya uchunguzi, aliuawa na daktari wa mifugo.
Msemaji alisema: "Tulihuzunika sana kuuliwa kwa Kuchakuro huyo huyu lakini tuliachwa bila chaguo kwa sababu ya mabadiliko ya sheria mnamo 2019 ambapo ni kinyume na sheria kumpeleka kindi porini.
"Sisi hatukubaliani na sheria hii na tukaipinga, lakini kisheria tunapaswa kuizingatia. Kuna njia nyingi za kibinadamu za kuwazuia kindi na tungesisitiza watu wasiwatege kwani sasa ni kinyume na sheria kuwaachia kurudi porini na chaguo pekee ni kuwaweka usingizini."
"Nilikuwa nikimwita rafiki mdogo kila nilipomwona kwenye bustani," Bi Reynolds alisema.
"Lakini baada ya haya yote kuanza kutokea, ndipo nilipobadilisha na kumuita Stripe.
"Nina huzuni kwamba kindi amepoteza maisha yake, lakini hakuna kitu kingine ambacho ningeweza kufanya. Uharibifu aliosababisha ulikuwa wa kushangaza."
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin