Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Stephen Masele ameonesha kusikitishwa na mvutano unaendelea miongoni mwa Makada wa CCM akiwemo Hamphrey Polepole na wengine akiwemo Nape Nnauye.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter,Masele ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) ameandika ujumbe ufuatao:
"CCM ni Chama kikubwa na chenye heshima na historia ya kipekee duniani. Ni vyema viongozi wakarejea kwenye misingi ya chama. wanapotofautiana kimitazamo. Ni vyema wakatumia lugha ya staha na kuheshimiana.Tunapeleka taswira mbaya kwa jamii tunayoingoza.Tujifunze kuvumiliana" . https://t.co/GzEDMWoBZ8
Social Plugin