Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limemkamata mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Edson Mathayo (33) mkazi wa Ndalla Tabora akituhumiwa kukutwa na noti bandia 17 ambazo ni dola za Kimarekani $4600 (sawa na Tsh milioni 10.6).
Akizungumza na waadishi wa habari leo Alhamisi, Desemba 30, 2021, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara amekamatwa leo wakati akienda kubadilisha Dola hizo bandia katika tawi la benki lililopo Manispaa ya Tabora.
“Mfanyabiashara huyo alienda kubadilisha Dola hizo na ndipo alipokamatwa kabla ya kutimiza azma yake ”, amesema Kamanda Abwao.
Social Plugin