Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa, Elizabeth Amos, aliyeuawa
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Naftali Lulandala, mkazi wa kijiji cha Uhambingeto kwa tuhuma za mauji ya mchungaji wa KKKT dayosisi ya Iringa Elizabeth Amos, baada ya kuingia tamaa ya fedha na kumpora marehemu huyo kiasi cha shilingi milioni 2 kabla hajamuua.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi, amesema tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Kipanduka wilayani kilolo mkoani Iringa ambapo marehemu alienda kwa ajili ya kufanya shughuli za usimamizi wa shamba wilayani humo.
Chanzo - EATV
Social Plugin