Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MFALME WA SHETANI MWENYE WAKE 57 HAJUI IDADI YA WATOTO WAKE AZIKWA KWENYE GARI


MWANAUME mmoja nchini Nigeria Simon Odo (74) maarufu kama ‘Mfalme wa Shetani’ amezikwa ndani ya gari katika Kijiji chake kusini mashariki mwa jimbo la Enugu baada ya kifo chake.

Mashine ya gari lake ilikuwa imewashwa na wimbo wake alioupenda ulisikika katika gari hilo, ambalo lilihudumu kama jeneza lake , kulingana na wale waliokuwepo.

‘Yalikuwa mazishi ya kwanza ya aina hiyo kufanyika katika Kijiji cha Aji, walisema wakazi. Bwana Odo aliomba kuzikwa hivyo’ , alisema mwanawe Uchema Odo.

 Mazishi hayo ya gari lililokuwa likiunguruma yaliashiria kusafiri kwake hadi ulimwengu mwingine , baadhi ya wanawe walisema.

Baadhi ya watu wa familia yake waliohojiwa walisema kwamba bwana Odo alikuwa mtu mzuri ambaye alipinga maovu wakati alipokuwa akishirikiana na watu.

 Mtoto wake wa kiume Uchenna Odo alisema baba yake alifariki mwendo wa saa tisa mchana baada ya kuugua kwa muda mfupi.


Taarifa ya kifo cha “Mfalme wa Shetani” ilitolewa na mwanae Uchenna Odo kwa njia ya simu katika shirika la habari la BBC.

 Wakati wa mahojiano na BBC Igbo mwaka 2020, alisema alikuwa na wake 57 na hakufahamu idadi kamili ya watoto wake zake walimzalia na hata wajukuu.


Mganga huyo wa tiba asilia alisema alirithi ushetani kutoka kwa wazazi wake na mababu ambao pia walikuwa ni waabudu shetani.

 Anasema watu kutoka sehemu tofauti huzuru madhabahu yake kila wakati kupata ushauri ya kiroho ambao anasema hutenda vitendo vinavyowadhuru binadamu wengine.

Je Mfalme wa shetani ni nani?


Odo aliambia BBC hakujua idadi ya Watoto na wake alionao.


Alikuwa mganga wa kienyeji maarufu sana wakati wa maisha yake na alijulikana kama 'mfalme wa shetani.'


Katika mahojiano na BBC Igbo kabla ya kifo chake, Simon Odo alielezea kwamba , kwa kweli mimi ndio 'mfalme wa shetani'. Iwapo utanikumbusha nitaokolewa pia.


Alisema nyumbani kwake kwamba alijifunza kile anachokifanya.


Alizaliwa katika ukataloki na akaanza kazi yake kama mganga wa kienyeji.


''Nilibatizwa 1956 na nikaanza kujifunza ukatoliki kati ya mwaka 1959 to 1960."

Ni nini kilichokufanya kuwa mganga wa kienyeji?


Aliugua ugonjwa wa kifua kikuu kwa miaka mitano na inaaminika ni wakati huo ndiposa aligundua.


Baadaye aliambukizwa ugonjwa mwengine


''Wamekuwa wakipigana kwa miaka kadhaa. Nimekuwa sijiwezi kwa miaka mitano''.


Ulikuwa ugonjwa huu ambao ulimfanya mkubwa Simon Odo kuelekea katika kijiji cha Ijebu ambapo aligundua kwamba kumbe ni mwanadamu na sio ugonjwa kutoka kwa Mungu.


Madhabahu ya mfalme wa shetani

Madhabahu ya mfalme wa shetani


Alikuwa katika jela ya Ode kwa miaka saba ;kabla ya kurudi nyumbani kwao kutafuta matibabu.


Ana nguvu na uwezo wa kuua.


Alisema: Iwapo mtu atatuletea dola milioni mia tatu kumuua mtu ama kumpatia sumu amuue mtu yeyote, mwambie mtu huyo kwamba haiwezekani. ''Ile siku nitafanya hivyo nitafariki''.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com