Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI CHANDE AFANYA ZIARA YA KIKAZI TEA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Hamad Hassan Chande (katikati) akisikiliza taarifa kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Waziri Rajab Salum (Kushoto).

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Hamad Hassan Chande (kulia) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Menejimenti wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Hamad Hassan Chande (katikati mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti wa Mamlaka ya Elimu Tanzania.

******************************

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Hamad Hassan Chande, leo tarehe 28 Desemba 2021 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa lengo la kujifunza kuhusu utendaji wa TEA.

Mhe. Chande amepongeza utendaji mzuri wa TEA ambayo amesema imekuwa Taasisi ya kwanza ya Muungano aliyoitembelea toka alipoteuliwa kushika wadhifa wake. “Hii imekuwa taasisi yangu ya kwanza ya Muungano kuitembelea toka nilipoteuliwa kushika wadhifa huu na hiyo inatokana na utendaji wake mzuri” Amesema Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ufadhili wa miundombinu ya elimu unaofanywa na TEA ambapo thamani ya fedha inaendana na ubora wa kazi akitolea mfano ukarabati wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST) iliyopo Zanzibar ambayo ilikarabatiwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Waziri Rajab Salum, amemshukuru, Mhe. Chande na kuahidi kuwa TEA itaendelea kutekeleza miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu kwa ufanisi na weledi.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya umma inayofanya kazi chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Mamlaka inaratibu Mfuko wa Elimu wa Taifa ambao jukumu lake kuu ni kuongeza jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com