***************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amefungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa kihistoria,utamaduni na mambo ya kale ili waweze kupata ujuzi wa namna ya kuibua vivutio vipya vya utalii vitakavyoingizwa kwenye urithi wa dunia ili kendelea kuvutia watalii wengi zaidi.
Ameyasema hayo leo mara baada ya kufungua Mafunzo hayo yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Tanzania ni mwenyeji wa Mafunzo hayo na endapo watapata ujuzi sahihi utawawezesha wataalam hao kuweza kuingiza vivutio vyao kwenye orodha ya urithi wa Dunia.
“Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wataalam wanaohusiana na masuala ya kihistoria, utamaduni na mambo ya kale Barani Afrika ili wapeleke ujuzi katika nchi zao na kuweza kuibua maeneo mapya yatakayoweza kuingizwa kwenye urithi wa Dunia na UNESCO” Mhe. Masanja amefafanua.