Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma, amesema kwamba kuhusu watu wanaobeza PhD yake mitandaoni atalizungumzia jambo hilo kuanzia Ijumaa.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 8, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, alipoulizwa analipi la kusema baada ya watu wengi kumbeza tangu atunukiwe udaktari wa heshima katika siasa na uongozi kutoka Chuo cha Academy of Universal Global Peace cha Marekani.
"Bahati mbaya mimi siko mitandaoni na kuhusu wanaonibeza, mimi nitazungumza kuanzia Ijumaa, sasa hivi bado nasoma tu hayo mambo yao wanayoyaandika," amesema Musukuma.
Chanzo - EATV
Social Plugin