Polisi nchini India wamemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ambaye anaripotiwa kuoa wake 60 na wote wakimlipa mahari.
Abu Baker ambaye ni mwalimu kutoka Jamalpur nchini India, alitiwa mbaroni huko Purbadhala, Bangladesh, kufuatia malalamishi ya mke wake Rosy Khanum ambaye alidai alimlaghai.
Inaripotiwa katika kipindi cha miaka 25, Abu Baker alioa wake 60, na mke wake wa mwisho ana umri wa miaka 20
Ashtakiwa
Katika kuanika uovu wake, mkewe mwenye umri wa miaka 60 aliwasilisha kesi mahakamani, akidai kuwa Baker amemtelekeza na kutumia hati ghushi kuoa. Gazeti la Dhaka Tribune linaripoti kwamba Baker alimlaghai mke wake wa sasa kuwa ni mseja na kusema jina lake ni Shaheen Alam na akamwomba baba wa msichana huyo amlipe gharama za harusi.
Baker alikuwa ameitisha mahari ya KSh 20,0000 lakini baba yake msichana huyo alikataa ombi hilo na kutoa KSh90,000. Hata hivyo, baada ya kupokea mahari hiyo, alimkimbia mke wake na kumchochea mkewe kupiga ripoti katika Kituo cha Polisi cha Purbadhala.
"Sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ni kupata pesa za kuoa, na nilitaka kupata pesa kutoka kwa wake 59 niliowaoa hapo awali, na hakuna hata mmoja wao aliyejua," alisema Abu Baker.
Kulingana na mila na desturi ya Wahindi, bibi harusi ndiye hujilipia mahari yake kabla ya kufanya harusi na hivyo kupata riziki kutoka kwa mchumba wake.
Baker ambaye ni mwalimu, alikamatwa na polisi na kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo dhidi yake na kukiri kwamba alioa wake 60 katika kipindi cha miaka 25, na wote walimlipa mahari.
Kulingana na polisi, mwanaume huyo alikuwa akitumia herufi ghushi na majina feki kila mara alipojifanya kuwa hajaoa.
Alifichua kwama anaishi katika jiji moja na wake zake watatu na watoto saba
Chanzo - Tuko News