Happy Lazaro, Arusha
Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro, jijini Arusha,Janerose Dewasi(66) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na anayetuhumiwa ni mfanyakazi wake wa ndani.
Tukio hili limetokea siku chache baada ya mwanamke mwingine,Ruth Mmasi kubainika kuuawa eneo la Njiro pia na anayetuhumiwa ni mtoto wake wa kiume Patrick Mmasi(19)
Kamanda Masejo amesema imebainika mwanamke huyo ambaye alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo kwenye nyumba yake eneo la block D mwili wake umepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso kushoto.
"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo wao pekee na alimuajiri wiki moja iliyopita”amesema
Hata hivyo amesema mara baada ya mauwaji hayo mfanyakazi huyo ametoweka na anaendelea kusakwa.
Kamanda amesema jeshi la polisi linatoa wito kwa wenye nyumba kuwa makini na wafanyakazi wa ndani wanaowapa kazi kwa kujua historia zao.
Mmoja wa majirani wa nyumba hiyo,Mary Muchi alisema mfanyakazi huyo alikuwa hajulikani sana mtaani kwani ameanza kazi muda si mrefu.
“Hatujui lolote huyo kijana anatajwa Boniface alikuwa akiimsaidia huyu mama kazi zao na leo tumeshangaa kupata taarifa za kifo cha mama huyu”,amesema.
Social Plugin