NABII SHILAA AIPONZA WASAFI TV, YAPIGWA FAINI NA TCRA


Na Magrethy Katengu D ar es salaam

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imekitoza faini ya shilingi milioni mbili kituo cha utangazaji cha wasafi Tv kwa kosa la kurusha kipindi kisicho na maudhui yasiyofaa kwa jamii kupitia chaneli yake ya youtube


Akizunzungumza na waandishi wa habari Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui mamlaka ya mawasiliano TCRA Hansi Gunze amesema Novemba 1 2021 mtangazaji wao Jordani Mwasha katika chaneli ya youtube alifanya mahojiano na Nabii Shilaa ambaye alitoa kauli chafu kukejeli dini ya kikristo kwa kumuita Yesu tapeli alikuwa anapenda matajiri ambapo kitendo hicho ni uvunjaji wa kanuni za maudhui


Hata hivyo amesema kutokana na kitendo hicho cha kukashfu dini ya kikristo kituo hicho walishusha video zote na kuomba radhi kupitia kurasa zake za mtandaoni kwa watanzamaji wake hivyo pamoja na kukiri na kuomba radhi TCRA wamewapa onyo kali na kuwataka kuendelea kuomba radhi kwa jamii kupitia chaneli zao zote kwa kurusha tangazo litakalopigwa mara tatu kwa siku kuanzia saa nne asubuhi siku tatu mfululizo. 


Sanjari na hayo amekitaka chombo hicho kuhakikisha shughuli zake za kuhabarisha Umma wanazingatia kanuni na sheria zilizowekwa pamoja kuajiri wafanyakazi walio na weledi na wahariri mahiri ambao kabla ya habari kurushwa wanaipitia vizuri ili kuondoa ukakasi kwa jamii na sintofahamu kwa watazamaji.


"Niwaase kuhakikisha vipindi vya dini vyote viwe na wahariri mahiri wenye utaalamu waadilifu kwani kufanya hivyo kutawasadia kuepuka adhabu zisizo na tija"alisema Gunze.


Kwa upande wake mkurugenzi wa vipindi kituo cha wasafi Spensa Lameki ameishukuru Mamlaka hiyo na amekiri kutoruhusu kosa kama hilo kujirudia tena na adhabu walizopewa watazitimiza .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post