NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Serikali imesema imekubali mapendekezo 108 ya
mikataba ya Kimataifa ya haki za binadamu na itawasilisha taarifa ya nchi Februari
14 ,2022 na kuweka mfumo wa kushirikiana na Asasi za Kiraia.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju wakati akizungumza
katika kikao kazi cha wadau wa masuala ya haki za binadamu kwenye Sekta ya
Asasi za kiraia ambacho kimeratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu
kwa lengo la kupitia mapendekezo 252 yaliyotolewa na nchi wanachama wa Baraza la Umoja wa
Mataifa wa haki za binadamu kwa Tanzania.
Mpanju amesema mapendekeezo ambayo serikali imeyakubali ni
ya hatua ya kwanza hivyo mchakato huo
utakamilika mwezi februari mwakani kwa kutoa taarifa waliyoyakubali na
kuyakataa.
Amesema kwaniba ya Serikali wamerudi na
mapendekezo kwa lengo ya kuyasambaza yote 252 kwa wadau serikali,taasisi na
Mamlaka za Asasi za Kiraia ili kuyajadili na kupata mawazo na ushauri kisha watapeleka kwenye kikao cha
makatibu wakuu.
‘Sisi Wizara ya Katiba na Sheria tuko tayari
kufanya kazi kwa karibu sana na nyie kwa sababu sisi sote na nia ya serikali
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona watanzania wote wanazifikia
haki na kunufaika nazo na haki kwa ujumla zinandelezwa kwa maslahi ya Tanzania
na Makundi yote’amesema Mpanju
Awali akizungumza Mratibu Kitaifa wa Mtandao
wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC ) Onesmo Olengurumwa amesema Tanzania
imefanyiwa mapitio mara ya tatu ambapo 2011 ilikuwa ni mapitio ya kwanza na
ilipata mapendekezo 153 na kukubali 107 na mwaka 2016 walipokea 227 na kukubali
133 sawa na asilimia 58 na kwa mwaka 2021 imeshuka kwa asilimia.
‘Ukiangalia mapendekezo mengi ambayo
yamekataliwa kwa mfano Mapendekezo yanayohusiana na haki za kijamii ni
mawili,kuhusu haki za wafugaji ni moja,kuhusu uhuru wa kujieleza ni 18,na
mapendekezo yaliyokataliwa kuhusiana na haki za kiuchumi yalikataliwa na haki
za wanawake na masuala ya jinsia 13 yamekataliwa na mapendekezo 9’amesema
Mratibu wa THRDC Olengurumwa
Kwa upande wao wawakilishi wa mashiriki ya
haki za binadamu,akiwemo Mwakilishi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC)
Raymond Paul pamoja na Wilbert Muchunguz kutoka Taasisi ya Save the Children
wameipongeza Wizara kushughulikia mchakato huo utakaosaidia kufanya uboreshaji
wa maswala ya haki za bianadamu.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu kutoka maeneo tofauti nchini,wawakilishi kutoka Zanzibar pamoja na waratibu wa Kanda na wafanyakazi wa THRDC.
Social Plugin