Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI TAMISEMI DKT. FESTO DUGANGE ARIDHISHWA KASI YA UJENZI WA MADARASA, VITUO VYA AFYA SHINYANGA NA KISHAPU



Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akiangalia ubora wa madawati katika Shule ya Sekondari Ukenyenge wilayani Kishapu katika vyumba vya madarasa vipya ambavyo vimejengwa wa fedha ya UVIKO-19.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Dk, Festo Dugange ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa vituo vya afya, vyumba vya madarasa, katika Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Manispaa ya Shinyanga.

Dugange ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe mkoani Njombe, amebainisha hayo leo Desemba 23,2021 wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa vituo vya Afya na vyumba vya madarasa katika Halmashauri hizo mbili huku akiwa ameambatana na Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, wataalam na viongozi wa CCM.

Amesema baada ya kukagua ujenzi huo, ameridhishwa na majengo hayo pamoja na kasi yake, huku akiagiza yakamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa, ili mwaka 2022 yaanze kutoa huduma.

“Nimekagua ujenzi wa kituo vya Afya Negezi wilayani Kishapu, na Ihapa Oldshinyanga Manispaa ya Shinyanga, pamoja na ujenzi wa vyumba vya Madarasa, kweli Mkoa wa Shinyanga mmeupiga mwigi kwenye utekelezaji wa miradi hii ya maendeleo mko vizuri,”alisema Naibu Waziri Dugange.

“Ninacho waomba sasa mmalizie kuikamilisha ili mwakani ianze kutoa huduma kama maagizo ya Serikali yanavyosema, na kwa kasi hii mliyonayo na imani mtakamilisha kwa wakati, na ukiangalia hata ujenzi wa vyumba vya madarasa vingi mmekamilisha pamoja na kuweka madawati,”aliongeza.

Aidha, aliziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani, pamoja na kutenga kiasi cha fedha asilimia 40 za mapato hayo, na kuzielekeza kwenye ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ilianzishwa kwa nguvu za wananchi yakiwamo Maboma ya Zahanati na vituo vya Afya.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo, alionya ubadhirifu wa fedha kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ukiwemo wizi wa saruji, ili miradi hiyo itekelezwe kwa ubora unaotakiwa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo, akizungumza kwenye ziara hiyo, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya na vyumba vya madarasa, huku akiahidi kusimamia miradi hiyo isihujumiwe.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, walimhakikishia Naibu Waziri huyo, kuwa miradi yote ya maendeleo wataisimamia vizuri, na kutekelezwa kwa ubora unaotakiwa, na kukamilika kwa wakati ndani ya muda uliopangwa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua ujenzi wa vituo vya Afya na vyumba vya Madarasa Manispaa ya Shinyanga na wilaya ya Kishapu.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, akizungumza kwenye ziara ya Naibu Waziri (TAMISEMI)Dk. Festo Dugange.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (katikati) akizungumza kwenye ziara hiyo ya Naibu Waziri (TAMISEMI) Dk, Festo Dugange.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, (kulia) akizungumza kwenye ziara ya Naibu Waziri (TAMISEMI)Dk, Festo Dugange, (kushoto) wakati alipowasili wilayani humo kukagua ujenzi wa kituo cha Afya Negezi na vyumba vya Madarasa.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Naibu Waziri (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye ziara hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Negezi wilayani Kishapu.
Muonekano ujenzi kituo cha Afya Negezi wilayani Kishapu.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule ya Sekondari Ukenyenge wilayani Kishapu.

Ukaguzi ubora wa Madawati ukiendelea ambapo Naibu Waziri (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange alilidhika na ubora wake.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Oldshinyanga.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Ihapa Oldshinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Awali Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akipanga Mti katika Shule ya Sekondari Ukenyenge wilayani Kishapu.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akipanda mti katika Shule ya Sekondari Ukenyenge wilayani Kishapu.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasilia Shinyanga kwa ajili ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwamo ujenzi wa vituo vya Afya na vyumba vya Madarasa. kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, (watatu kushoto)akiwa katika ziara ya ukaguzi wa kituo cha Afya Ihapa Oldshinyanga, (wapili kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com