Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliofariki kufuatia kula samaki wa aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu huko Matemwe, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuzinasihi familia za marehemu hao kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hichi kigumu cha msiba pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwaponya kwa haraka waliodhurika baada ya kula samaki huyo.
Rais Dk. Mwinyi katika salamu hizo za rambirambi, amesema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake husika itaendelea kuhakikisha wale wote waliodhurika wanaendelea kupatiwa tiba ili waweze kurudi katika hali zao nzuri za kiafya.
Social Plugin