Waziri Bashungwa akipokea Tuzo ya Heshima kwa Niaba ya Rais wa Tanzania, Rais Samia kwa kutambua mchango wake wa kuiendeleza Tasnia ya Filamu nchini ikiwemo “Royal Tour”.
Tuzo za Filamu Tanzania zimefanyika Disemba 18, 2021 katika ukumbi wa Tughimbe mkoani Mbeya chini ya Usimamizi wa Bodi ya Filamu Tanzania.
Waziri Wamichezo, Sanaa na Utamaduni, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa mikoa yote nchini kuiga Mkoa wa Mbeya katika kushirikiana na Wizara yake kuandaa Tuzo za Filamu katika miaka ijayo ili kukuza vipaji na kutoa ajira kwa wasanii wengi zaidi walio kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini.
Waziri Bashungwa amepokea Tuzo ya Heshima kwa Niaba ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kutambua mchango wake wa kuiendeleza Tasnia ya Filamu nchini ikiwemo “Royal Tour”.
Social Plugin