RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuna makundi ya watu ndani ya Serikali wamekuwa wakifanya mambo ya hovyo jambo ambalo linarudisha nyuma utendaji wa Serikali.
Mhe. Samia amesema hayo leo Jumamosi, Desemba 4, 2021 wakati akizungumza alipohudhuria uzinduzi wa maboresho ya gati namba 1 hadi namba 7 ya Bandari Kuu ya Dar es Salaam.
“Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali…ni makundi hayo hayo yanageuka kusema serikali awamu ya sita ufisadi umerudi, mambo yako hovyo…kumbe wao ndio wako hovyo.
“Na mambo yale hayakufanyika ndani ya awamu ya sita… yalifanyika huko nyuma, gari bovu linaangushiwa awamu ya sita… sitakubalii… sitakubali…,” amesema Rais Samia.
Chanzo - Global Publishers
Social Plugin